Unganishwa

Search the region

22855 stories

Uncategorized · Business Daily

How hospitals will be licensed under new SHA rules

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Catalan separatist Puigdemont cleared to return to Spain

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

Archbishop Kiwanuka Empowerment Centre Receives UGX 30 Million Boost from dfcu Bank

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

Pearl Bank Confirms Steven Mwesige as Chief Information Security Officer

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

KMPDU demands urgent protection for health workers after Kenya confirms first Ebola case

Latest · Capital Health

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

EU delegation explores investment opportunities in Kiambu

The delegation said the main goal is to improve and make close relations between the EU and Kenya

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KIWANDA CHA VILIPUZI KISARAWE KITAPUNGUZA UTEGEMEZI WA BIDHAA KUTOKA NJE - NYONGO

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema uwepo wa kiwanda cha baruti na vilipuzi cha Ideal Detonators Tanzania Limited wilayani Kisarawe utasaidia kupunguza gharama na utegemezi wa uagizaji wa bidhaa hizo kutoka nje ya nchi. Nyongo amesema bidhaa hizo ni muhimu katika shughuli mbalimbali za miundombinu, ikiwemo ulipuaji wa miamba na uchimbaji wa madini, hivyo uzalishaji wake nchini utasaidia kurahisisha upatikanaji wake. Ameyasema hayo Oktoba 6, 2026, baada ya kukagua kiwanda hicho wakati wa ziara yake wilayani Kisarawe, ambapo alisema miaka ya nyuma hakukuwa na sheria zilizowezesha ujenzi wa viwanda vya kutengeneza vilipuzi nchini. Hata hivyo, alisema Serikali imefanya maboresho ya sheria na kuweka mazingira yaliyowezesha kuanzishwa kwa viwanda hivyo nchini. Nyongo aliishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira yaliyowezesha uwekezaji huo, akisisitiza kuwa Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa yenye fursa kubwa za viwanda na uwekezaji. Alisema mkoa utaendelea kushirikiana na halmashauri kuhakikisha wawekezaji wanapata mazingira rafiki ya uzalishaji, ikiwemo upatikanaji wa huduma muhimu za maji na umeme. Aidha, Nyongo amekemea uvamizi wa maeneo ya wawekezaji na migogoro ya ardhi, huku akiwataka viongozi, wakiwemo wabunge, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uwekezaji badala ya kuwa vikwazo kwa wawekezaji. Kwa upande wake, Mbunge wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, alisema kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwa vijana, hususan wazawa, pamoja na kuongeza mapato na kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo hilo. Jafo pia alisema uwepo wa kituo cha kupoozea umeme katika eneo hilo utasaidia kuongeza uwezo wa usambazaji wa umeme katika maeneo mbalimbali. Alipongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini kwa hatua zinazochukuliwa katika kuendeleza sekta hiyo, akisema uwekezaji huo unaonesha utekelezaji wa dhana ya kuongeza thamani ya madini kwa kuzalisha bidhaa zinazohitajika katika shughuli za uchimbaji badala ya kuishia kwenye uchimbaji pekee. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, alisema wilaya hiyo inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuharakisha ujenzi na uanzishaji wa viwanda. Alifafanua kuwa kwa sasa Kisarawe ina viwanda viwili vya baruti na vilipuzi, ambavyo ni Solar Intracom Chemicals (Solar Nitrochemicals Limited), ambacho tayari kimeanza uzalishaji, na Ideal Detonators Tanzania Limited, kinachoendelea na maandalizi ya kuanza uzalishaji. Magoti alisema Ideal Detonators ni miongoni mwa viwanda vikubwa vya aina hiyo katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku uwekezaji wake ukifikia zaidi ya Sh bilioni 15. “Wilaya hiyo iko tayari kwa mapinduzi makubwa ya viwanda na inatarajia kupokea uwekezaji mwingine katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, zikiwemo nondo, spika na viwanda vya kutotolesha kuku,” alisema Magoti. Meneja Mkuu wa Ideal Detonators Tanzania Limited, Ramadhan, alisema lengo la kiwanda hicho ni kutoa suluhisho la upatikanaji wa bidhaa za vilipuzi zinazohitajika katika shughuli za uchimbaji madini na shughuli nyingine zinazohitaji matumizi ya vilipuzi.

Tue, 06 Oct 2026 14:06:27 +0000
Business · Issa Michuzi

IOP YAWEZESHA JAMII KUPITIA MIRADI YA ELIMU, AFYA NA UJASIRIAMALI

NA DENIS MLOWE IRINGA SHIRIKA la Ilula Orphan Program (Tanzania) (IOP) limeeleza namna linavyotekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa lengo la kuboresha maisha ya jamii, hasa watoto, vijana, wanawake na wazee katika mikoa ya Iringa na wilaya ya Kilolo. Akizungumza na wanahabari, MkurugenziMtendaji wa . Shirika hilo wakati wa maonesho ya Wiki ya NGOs, ambapo lilieleza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kupitia miradi yake ya kijamii pamoja na miradi ya kujitegemea inayolenga kuhakikisha huduma zinaendelea hata pale ufadhili kutoka kwa wahisani unapopungua. Msigwa amesema kuwa miongoni mwa miradi ya kijamii inayotekelezwa ni kituo cha watoto kinachohudumia watoto 45, wakiwemo wasichana na wavulana, pamoja na mradi wa ufadhili wa elimu unaowezesha watoto kuanzia elimu ya awali hadi sekondari. Shirika hilo limeeleza kuwa kupitia mradi huo linawahudumia watoto 616 katika ngazi mbalimbali za elimu, hatua inayolenga kuwawezesha kupata elimu na mazingira bora ya kujifunzia. Aidha, IOP inaendesha mradi wa utoaji wa chakula cha mchana pamoja na msaada wa pembejeo za kilimo katika shule sita za msingi wilayani Kilolo. "Lengo la mradi huo ni kuwawezesha watoto kupata mahitaji muhimu wakiwa shuleni, hususan wale wanaotoka katika maeneo ya mbali na shule na ambao hukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kuathiri mahudhurio na ujifunzaji wao." Alisema Msigwa alisema kuwa katika eneo la kuwawezesha wasichana na akinamama waliopata ujauzito katika umri mdogo, IOP inaendesha programu inayolenga kuwasaidia kurejea katika maisha ya kawaida na kutimiza ndoto zao ambazo zinaweza kuwa zimesitishwa kutokana na changamoto walizokutana nazo. Ameongeza kuwa kwa sasa, shirika hilo lina akinamama sita wanaoishi katika nyumba maalumu huku wengine wakisaidiwa wakiwa majumbani kwao huku Programu hiyo inawahudumia wasichana na akinamama waliopata ujauzito katika umri mdogo, wakiwemo wenye umri wa miaka 14, 17 na 18, ambao wanakabiliwa na mazingira hatarishi. Alisema kuwa katika mwaka wa kwanza wa programu hiyo, wanufaika hupatiwa mafunzo, msaada wa kisaikolojia pamoja na elimu ya malezi na makuzi ya watoto huku katika miaka inayofuata, wanajengewa uwezo katika fani mbalimbali kulingana na vipaji na mahitaji yao, huku baadhi wakichagua kurejea shuleni na wengine kujifunza ujuzi wa kuwawezesha kujitegemea. Alisema kuwa shirika la IOP linaendesha mradi wa kuwawezesha wanawake na vijana katika wilaya za Iringa na Kilolo kwa kuwapatia fursa na ujuzi unaoweza kuwasaidia kujenga maisha yao na upande wa wazee, shirika hilo linaendesha mradi unaowahudumia wazee wenye umri wa miaka 70 na kuendelea, ambapo kwa sasa linawafikia wazee 69. Aliongeza kuwa IOP pia hufanya shughuli za utetezi kwa ajili ya wazee na kuwawezesha baadhi yao kupata bima za afya kulingana na mahitaji na hali zao ambapo mbali na miradi ya kijamii, IOP imesema imeanzisha miradi ya kujitegemea kutokana na kutokuwa na uhakika wa ufadhili kutoka kwa wahisani ambao wakati mwingine unaweza kukoma bila taarifa ya kutosha. Kutokana na hilo alisema kuwa kama IOP amekuwa na miradi ya kilimo, ambacho mbali na kuzalisha chakula kwa ajili ya shule na vituo vinavyomilikiwa na IOP, pia huzalisha mazao ya ziada yanayouzwa ili kupata mapato. Shirika hilo pia linaendesha ufugaji wa kuku na uzalishaji wa maziwa, ambapo sehemu ya maziwa hutumika kulisha watoto wanaohudumiwa na IOP na sehemu nyingine huuzwa katika migahawa kwa ajili ya kupata mapato. Aidha, IOP ina karakana inayohusika na utengenezaji wa samani kwa ajili ya matumizi ya ndani na kuuzwa nje, pamoja na kufanya ukarabati wa majengo ya shirika ,pia linaendesha taasisi za elimu zikiwemo shule ya awali, shule ya sekondari na chuo, ambazo ni sehemu ya juhudi zake za kuchangia maendeleo ya elimu na kujenga uwezo wa jamii.

Tue, 06 Oct 2026 14:08:58 +0000
Uncategorized · The Exchange Rwanda

Kenya confirms first imported Bundibugyo Ebola case as patient dies in Nairobi

Read the full report from the original source.

Recently
National · Issa Michuzi

NYONGO-BUNGE LIANGALIE UPYA SHERIA NA TARATIBU ZA MANUNUZI KUEPUKA KUCHELEWA KWA MIRADI

Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe MKUU wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, ameliomba Bunge kuangalia upya sheria na taratibu za manunuzi ili kurahisisha upatikanaji wa fedha na vifaa vya miradi ya maendeleo, akisema ucheleweshaji wake unasababisha miradi kutokamilika kwa wakati. Nyongo alitoa ombi hilo Oktoba 6, 2026, baada ya kukagua ujenzi wa Chuo cha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa katika Kata ya Kazimzumbwi, wilayani Kisarawe. Alisema moja ya changamoto zinazokwamisha kasi ya ujenzi wa chuo hicho ni ucheleweshaji wa fedha pamoja na taratibu za manunuzi, hali inayosababisha baadhi ya kazi kusuasua. “Kuna umuhimu wa kurahisisha mchakato wa manunuzi pale fedha za mradi zinapokuwa tayari, ili utekelezaji uweze kwenda kwa kasi na miradi ikamilike kwa wakati,” alisema Nyongo. Alieleza kuwa ujenzi wa chuo hicho ulitarajiwa kukamilika mwaka 2023, lakini umekumbwa na changamoto mbalimbali zilizosababisha kuchelewa, huku akipongeza kasi ya utekelezaji iliyopo kwa sasa. Nyongo alisema kuongezeka kwa viwanda wilayani Kisarawe kunahitaji uwepo wa vijana wenye ujuzi wa ufundi, hivyo kukamilika kwa chuo hicho kutasaidia kuzalisha wataalamu watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira na viwanda vinavyoendelea kuanzishwa wilayani humo. Kwa upande wake, Mhandisi Mshauri wa mradi huo, Saidi Masoud Kisiki, alisema mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili, ambapo awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa majengo tisa. “Ujenzi umefikia asilimia 68.3, huku kazi katika majengo manane ikiwa imesimama kusubiri vifaa ambavyo mchakato wa manunuzi yake unaendelea katika ngazi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST),” alisema. Aliongeza kuwa mradi huo pia unakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa maji, barabara na umeme. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, alisema tayari wamewasiliana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuhusu changamoto ya barabara inayoelekea chuoni hapo na kwamba hatua za kuishughulikia zinaendelea. Magoti alisema kukamilika kwa chuo hicho kutakuwa na manufaa makubwa kwa vijana wa Kisarawe kwa kuwa kitawapa fursa ya kupata elimu ya ufundi na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri. Naye Mbunge wa Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, alisema vyuo vya VETA vina nafasi muhimu katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuwapatia elimu ya vitendo na ujuzi unaowawezesha kujiajiri, kuajiriwa au kuajiri wengine. Jafo alisema chuo hicho ni fursa kubwa kwa vijana wa Kisarawe kupata ujuzi katika fani mbalimbali na kutumia ujuzi huo kujikwamua kiuchumi.

Tue, 06 Oct 2026 14:02:10 +0000
Uncategorized · UN News Burundi

‘The clock on AI regulation is ticking’, warns UN rights chief

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Germany news: Saxony-Anhalt elects AfD parliamentary speaker

Read the full report from the original source.

Recently
Technology · Issa Michuzi

Yas yapokea cheti cha shukrani katika kilele cha Tech & AI Expo Zanzibar 2026

Kampuni ya mawasiliano ya Yas Tanzania imepokea cheti cha shukrani katika hafla ya chakula cha jioni ya kufunga maonesho ya Tech & AI Expo Zanzibar 2026, yaliyowakutanisha wadau wa teknolojia, wabunifu na viongozi kujadili maendeleo ya uchumi wa kidijitali visiwani Zanzibar hivi karibuni. Cheti hicho kilikabidhiwa na Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Ubunifu Zanzibar, Mudrick Ramadhan Soraga, na kupokelewa na Afisa Mkuu wa Yas Business, Norman Kiondo. Waziri Soraga aliishukuru Yas kwa kuwa mdhamini mkuu wa tukio hilo. Katika hafla hiyo, pia alikabidhi tuzo kwa washindi wa shindano la Hackathon na washiriki wa mijadala. Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Soraga alisisitiza dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukuza ubunifu, teknolojia na matumizi ya akili bandia ili kuendeleza uchumi wa kidijitali. Kwa upande wake Bw. Norman Kiondo - Afisa Mkuu wa Kitengo cha Yas Business alisema “Tunashukuru kwa kutambuliwa kwa mchango wetu katika maonesho haya. Yas itaendelea kuwekeza katika miundombinu na huduma za kidijitali Zanzibar ili kuwasaidia wananchi na biashara kutumia teknolojia katika shughuli zao za kila siku. Tunaamini ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wabunifu ni muhimu katika kufanikisha maendeleo ya Zanzibar,” alisema Kiondo.

Tue, 06 Oct 2026 11:00:00 +0000
Uncategorized · Citizen Digital

KMPDU demands transparency, protection of health workers after first Ebola case reported

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Nigeria mourns 25 killed as military plane crashes into swamp

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Africa CDC deploys emergency team to Kenya after first Bundibugyo Ebola case

Latest · Africa

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

WHH améliore l’accès à l’eau et à l’hygiène dans 13 écoles

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Standard

Mutiso murder: Ndetei says life in danger, opposes bail for ex-wife Mbithe and children

In his affidavit, Ndetei claimed that he had been intimidated by Mbithe and their children for more than 30 years.

Tue, 06 Oct 2026 16:30:00 +0300
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

L’UNIPROBA appelle à renforcer la scolarisation des enfants Batwa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Agence Burundaise de Presse

Les conflits familiaux peuvent laisser des séquelles durables chez l’enfant, selon un psychologue clinicien

Read the full report from the original source.

Recently

Page 839 of 1143 · 22855 stories