Search the region
22855 stories
PS: Health authorities will contain Ebola
Kenya confirmed first Ebola case on Tuesday of patient who travelled from DRC
RecentlyNdejembi graces CATA conference, insists on the use of digital technology for tax administration
Read the full report from the original source.
RecentlyWAZIRI AKWILAPO ATOA RAI MAANDALIZI YA EL NIÑO KULINDA MAKAZI
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, ametoa rai kwa mamlaka za miji, taasisi na wananchi kuanza kuchukua hatua za maandalizi dhidi ya athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua za El Niño na kusisitiza umuhimu wa upangaji bora wa maeneo ya makazi na uimarishaji miundombinu. Dkt. Akwilapo ametoa rai hiyo Oktoba 5, 2026 jijjni Dodoma wakati akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani 2026, yaliyofanyika chini ya kaulimbiu isemayo Makazi Toshelezi kwa Wote. Amesema, uzoefu wa mafuriko yaliyowahi kutokea nchini ni ukumbusho wa umuhimu wa kuchukua hatua mapema ili kulinda maisha ya wananchi, makazi na miundombinu. “Tusisubiri mvua inyeshe ndipo tuanze kuchukua hatua, kila mmoja wetu aanze sasa. Mamlaka za miji na taasisi zote zizingatie hatua zote kama zilivyoelekezwa na mamlaka za nchi ili kupunguza athari za janga hili,” amesema Dkt. Akwilapo. Akizungumzia makazi bora, Dkt. Akwilapo amesema, makazi toshelezi hayamaanishi kuwa na nyumba pekee, bali yanahusisha nyumba salama, ardhi iliyopangwa, huduma muhimu, usalama wa miliki, miundombinu imara pamoja na mazingira yanayoweza kustahimili changamoto za mazingira na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo, amesema ongezeko la watu na kasi ya upanuzi wa miji nchini linahitaji mipango madhubuti ya kuhakikisha maeneo ya makazi yanapangwa na kuendelezwa kwa kuzingatia usalama wa wananchi na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza, ikiwemo mafuriko.“Uzoefu wa mafuriko unatukumbusha umuhimu wa kupanga vizuri, kujenga kwa usalama, kutunza mazingira na kuimarisha miundombinu” amesema. Ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha maendeleo ya makazi na miji, ikiwemo mchakato wa maboresho ya Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi ya mwaka 2000 ili iendane na mahitaji na changamoto za Tanzania ya sasa. Kwa mujibu wa Dkt. Akwilapo, juhudi za Serikali katika kuboresha miji zinaenda sambamba na utekelezaji Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, Ajenda Mpya ya Miji na Lengo la 11 la Maendeleo Endelevu (SDG 11), linalolenga miji na makazi kuwa jumuishi, salama, himilivu na endelevu. Ametoa wito kwa Serikali, sekta binafsi, taasisi za fedha, vyuo na taasisi za utafiti, mashirika ya kimataifa, washirika wa maendeleo na wananchi kushirikiana kuhakikisha Tanzania inajenga makazi salama, bora, yanayomudu gharama na yanayostahimili changamoto za sasa na zijazo. Awali Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga ameielezea Siku ya Makazi Duniani kuwa inatoa fursa ya kutafakari kwa pamoja kuhusu hali ya makazi nchini, mafanikio yaliyopatikana na changamoto zilizopo na hatua zinazoweza kuchukuliwa ili kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora salama na ya gharama nafuu. Kwa upande wake Mwakilishi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani nchini Tanzania Dkt. Grace Lubaale amesema wakati dunia ikiadhimisha siku ya Makazi duniani Tanzania inaendelea kukua kwa kasi huku miji nayo ikiendelea kupanuka. "Ukuaji huu unaongeza mahitaji ya nyumba, ardhi iliyopangwa, miundombinu na huduma za msingi, hivyo tunahitaji kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na wadau mbalimbali katika kutafuta kwa pamoja suluhisho kwa pamoja "kidole kimoja hakivunji chawa"amesema. Siku ya Makazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Jumatatu ya kwanza ya mwezi Oktoba ambapo kwa mwaka huu wa 2026 siku hiyo imeadhimishwa Oktoba 5, 2026. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani Oktoba 5, 2026 jijini Dodoma Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani Oktoba 5, 2026 jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze. Mwakilishi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani nchini Tanzania Dkt. Grace Lubaale akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani Oktoba 5, 2026 jijini Dodoma. Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Makazi wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Deogratias Kalimenze akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Anthony Sanga katika Madhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma Oktoba 5, 2026. Sehemu ya washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma Oktoba 5, 2026 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo (Katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika jijini Dodoma Oktoba 5, 2026. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Tue, 06 Oct 2026 13:37:07 +0000Hali ya hewa itakavyokuwa leo na kesho kwenye Mkoa wako
Soma zaidi hapa...
RecentlyPS: Health authorities will contain Ebola outbreak
Kenya confirmed first Ebola case on Tuesday of patient who travelled from DRC
RecentlyNMB yapeleka fursa za uwekezaji Tanzania London
Read the full report from the original source.
RecentlyTPLB Yaja na ‘Gas Detector’, Mashabiki wa Simba SC na Yanga SC watambiana kuelekea Kariakoo Derby.
VIWANJANI : Mashabiki wa Simba SC na Yanga SC watambiana kuelekea Dabi ya Kariakoo ya Ligi Kuu ya NBC itakayopigwa Oktoba 10, 2026, huku mmoja wa mashabiki akimtaja mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Doumbia kuwa ndiye mchezaji bora nchini kwa sasa. Mjadala huo umeibua hoja mbalimbali kutoka kwa mashabiki wa timu hizo kuhusu timu itakayoondoka na alama tatu muhimu. Azam TV
2026-10-06T13:14:28+00:00Le premier ministre visite plusieurs départements communaux
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya’s Ebola Tools Face Their First Real Test
Read the full report from the original source.
RecentlyTuwaepushe wanafunzi dhidi ya ukatili
Read the full report from the original source.
RecentlyJambojet supports Ebola contact tracing after Kenya reports first case
Read the full report from the original source.
RecentlyAppel à une synergie d’action dans la lutte contre les VBG
Read the full report from the original source.
RecentlyBurundi : OCHA alerte sur le risque d’épidémies
Read the full report from the original source.
RecentlyGisyo-Kibenga : les habitants réclament un pont sur la rivière Kanyosha
Read the full report from the original source.
RecentlyUmuhanzi Bwiza agiye gutaramira abo muri Zambiya
Read the full report from the original source.
RecentlyCHIMP SPORT: Inhensiko Takes Next Step Towards Swimming Dream
Read the full report from the original source.
RecentlyKenya Confirms First Ebola Death
Read the full report from the original source.
RecentlyQ & A: Amb Nimisha Madhvani: Clear Incentives, Less Red Tape Key in Attracting Foreign Capital, Diaspora Wealth
Economic and commercial diplomacy increasingly places trade, investment, tourism and technology partnerships a..
RecentlyPM Nabbanja meets Development Partners ahead of National Partnership Forum
Read the full report from the original source.
RecentlyMakamu wa Rais afungua mkutano wa Chama cha Wasimamizi wa kodi wa Jumuiya ya Madola
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 840 of 1143 · 22855 stories