Search the region
22794 stories
Mambo 3 ya kimkakati kufanya eneo vita vya Majimaji ilikoanzia kuwa Urithi wa Dunia
Na Mwandishi Wetu, Kilwa MAMBO makubwa matatu ya kimkakati yametekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii katika kuwezesha eneo lenye utajiri wa historia ya namna vita vya Majimaji ilivyoanza kupiganwa Julai 15, 1905 katika vijiji vya Nandete na Kibata, Kata ya Kipatimu, wilayani Kilwa mkoani Lindi yanaingizwa kwenye orodha ya maeneo yaliyo katika Urithi wa Dunia. Tayari eneo hilo muhimu lenye kumbukumbu kadhaa ikiwemo mche wa pamba, zao ambalo ndilo lilikuwa chanzo cha kuanza kwa vita hivyo, mapango yaliyotumika kujificha, nyumba za asili za kabila la Wamatumbi, Boma aliloishi Mjerumani na kisima cha maji alichotumia Mjerumani yameingizwa kwenye orodha ya Urithi wa Taifa. Utekelezaji wa mambo hayo matatu ya kimkakati umetajwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Malikale katika Wizara ya Maliasili na Utalii, William Mwita wakati akitoa salamu za Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi kwenye kilele cha Maadhimisho ya Miaka 121 ya Kuanza kwa Vita vya Majimaji yaliyofanyika katika Kijiji cha Nandete juzi. Mambo yaliyotekelezwa kwa kiwango cha juu na Wizara ya Maliasili na Utalii hadi sasa ni pamoja na kuanza kuandikwa upya kwa historia ya kuanza kwa vita hivyo ili kueleza kwa ufasaha mahali, sababu na namna vita hivyo vilivyoanza na kupiganwa katika eneo hilo la Nandete kabla ya kusambaa nchi nzima na kuhitimishwa mkoani Ruvuma. Baada ya kuanza katika eneo hilo la Nandete mkoani Lindi baada ya Wamatumbi kupinga unyanyasi uliokuwa unafanywa na Utawala wa Mjerumani kwa kuwatumikisha katika mashamba ya pamba, vita hivyo vilisambaa katika mikoa ya Mtwara, Pwani, Dar es Salaam, Morogoro, Iringa na hatimaye Ruvuma ilikotamatika Agosti 8, 1907. Jambo la pili la kimkakati lililotekelezwa ni kuanza kufungamanisha mnyororo mzima wa maeneo ambayo vita hivyo vilipiganwa kwa kuanzisha maadhimisho ya kumbukizi kwa lengo la kuenzi tunu na ushujaa uliofanywa na wazee wa maeneo hayo katika kulipigania Taifa lao kama sehemu ya kuamsha ujasiri, umoja, mshikamo na uzalendo kwa vizazi vya sasa katika kulilinda Taifa lao kwa wivu mkubwa. Jambo la tatu ambalo pia limetekelezwa kwa ufanisi mkubwa ni ujenzi wa Kituo cha Kukusanya taarifa kuhusu Kuanza kwa Vita vya Majimaji kilichopo katika Kijiji cha Nandete ambapo serikali imetoa takribani Sh bilioni 1.3 ili kugharamia ujenzi wake, kikitarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mapema mwaka 2027. Mkurugenzi Msaidizi Mwita anasema hatua hiyo mbali ya kuwezesha eneo hilo kutambuliwa kama sehemu ya urithi wa dunia, kukamilika kwa program hizo zinazoendelea kuchukuliwa kutawezesha pia kukuza utalii katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania, kukuza ajira, kuinua uchumi wa nchi, kujenga Taifa la vijana wanaojua nchi imetoka wapi na inakokwenda na hivyo kujenga uzalendo, umoja na mshikamano wa kitaifa.
Mon, 05 Oct 2026 09:27:31 +0000Un logement décent, un défi pour les déplacés au Cameroun
Read the full report from the original source.
RecentlyLe Burundi et la Tanzanie renforcent leur coopération dans plusieurs secteurs
Le Burundi et la Tanzanie ont franchi une nouvelle étape dans le renforcement de leur coopération bilatérale. Le mercredi 30 septembre 2026, les Ministres en charge des Affaires étrangères des deux pays, Édouard Bizimana du Burundi et Mahmoud Thabit Kombo de...
Mon, 05 Oct 2026 09:24:36 +0000IEBC puts parties on notice over gender balance in 2027 nominations
News · Quick read
RecentlyCS Wahome: Dangote Lamu refinery to be built on govt-owned land
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyOgamba to dons: Obey court orders and return to work
Ogamba said the government remains committed to resolving their grievances through negotiations.
RecentlyWhy Tanzania’s ‘ndugu’ can become the most powerful language of peace and diplomacy today
ITALY: On October 4, the Catholic Church commemorate the life and legacy of St. Francis of Assisi, a figure whose…
RecentlyHigh Court blocks JSC move to have tribunal investigate Justice Ombwayo
Latest · NATIONAL NEWS
RecentlyNDG. ABDI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA WA VIUNGO KIZIMBANI
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, ameahidi kushirikiana na taasisi husika kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa bidhaa za viungo (Spice) katika eneo la Kizimbani, Zanzibar. Ndugu Abdi ametoa ahadi hiyo baada ya kuwatembelea wafanyabiashara hao katika eneo lao la biashara, ambapo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuendesha shughuli zao na kujikwamua kiuchumi. Amesema changamoto zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao zitafanyiwa kazi kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika, ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na kuwawezesha kuendeleza shughuli zao za kiuchumi. Kwa upande wao, wafanyabiashara hao wamemuomba Ndugu Abdi kuwasaidia katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa mikopo, ambayo itawawezesha kuongeza mitaji, kupanua biashara zao na kuongeza fursa za ajira kwa vijana. Wamesema upatikanaji wa mitaji ya kutosha utawasaidia kuongeza uzalishaji na kukuza biashara ya bidhaa za viungo, ambayo ni miongoni mwa shughuli zinazowapatia kipato na kuchangia katika uchumi wa Zanzibar.
Mon, 05 Oct 2026 09:17:12 +0000Housing crisis threatens Africa’s health and economic prospects
Read the full report from the original source.
RecentlyCS Ogamba urges university lecturers to resume work, pledges to conclude 2025/2029 CBA talks
NATIONAL NEWS · 4 hours ago
RecentlyTADB kupeleka 14 maonesho Japan
Read the full report from the original source.
RecentlyCRDB BANK FOUNDATION YASHIRIKI JUHUDI ZA KIMATAIFA KUFIKISHA MITAJI VIJIJINI
Na Mwandishi Wetu. Rome, Italia. Tarehe 4 Oktoba 2026: Taasisi ya CRDB Bank Foundation imeendelea kujiimarisha kama daraja muhimu la mitaji ya kimataifa na jamii ambazo hazijafikiwa ipasavyo na huduma za fedha, baada ya kushiriki mkutano unaojadili Ufadhili Mseto wa Miradi yaani Blended Finance Working Group (BFWG) ulioandaliwa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa fedha kwa wananchi na biashara za vijijini. Akishiriki mkutano huo uliowajumuisha wadau wengine ukiwamo Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Ujasiriamali ya Uholanzi (FMO), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), pamoja na wadau wa maendeleo, taasisi za fedha na wataalamu wa sekta mbalimbali, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amesema mikakati ya pamoja inahitajika kuwafikia wananchi wenye uhitaji wa mitaji nafuu ili nao washiriki kuujenga uchumi wa mataifa yao. Akizungumza pembezoni mwa mkutano huo, Tully amesema CRDB Bank Foundation ipo katika nafasi ya kipekee ya kuunganisha rasilimali za kimataifa na fursa zilizopo katika jamii kwa sababu ya uelewa wake wa kina kuhusu mahitaji ya wananchi wa vijijini pamoja na dhamira yake ya muda mrefu ya kukuza ujumuishaji wa kiuchumi. "Upatikanaji wa fedha bado ni moja ya changamoto kubwa kwa jamii za vijijini na biashara ndogondogo. Kupitia uzoefu wetu chini ya Programu ya iMBEJU Kilimo, tumedhihirisha kuwa ushirikiano sahihi na mifumo bunifu ya ufadhili, inaweza kurahisisha namna kuwafikia wananchi ambao mara nyingi huonekana kutofikika na huduma za kifedha na kuwasaidia kuwa washiriki wenye tija katika uchumi," amesema. Majadiliano ya mkutano huo yalijikita katika kutafuta majibu ya swali muhimu kuhusu namna ya kuhamasisha na kuelekeza mitaji zaidi kwa jamii, wakulima na biashara zinazohitaji fedha ili kukuza shughuli zao za kiuchumi hivyo kutoa fursa kwa washiriki kubadilishana uzoefu kuhusu mchango wa mifumo ya ufadhili mseto (blended finance), dhamana za mikopo, na nafasi ya taasisi imara za fedha katika kuvutia uwekezaji mkubwa zaidi kwenye sekta za kilimo na maendeleo ya biashara za vijijini. Majadiliano hayo pia yalisisitiza umuhimu wa kuziba pengo lililopo kati ya wawekezaji wa kimataifa na jamii nyingi ambazo bado zimeendelea kubaki nje ya mifumo rasmi ya fedha. Kwa CRDB Bank Foundation, ushiriki katika mikutano ya BFWG umetoa jukwaa muhimu la kushirikisha uzoefu wa Tanzania katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati unaoweza kuleta vyanzo vipya vya mitaji karibu zaidi na wajasiriamali wa vijijini, wakulima na biashara zinazomilikiwa na jamii. Zaidi ya hayo, Foundation inaendelea kuonyesha dhamira yake ya kuziba mapengo ya upatikanaji wa huduma muhimu za maendeleo kama inavyofanya sasa kupitia programu ya iMBEJU Nuru, inayotekelezwa kwa ushirikiano na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kutoa ruzuku za gharama za kuunganishiwa umeme kwa jamii za vijijini ambazo zina changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu. Kupitia mipango kama hii, CRDB Bank Foundation inaendelea kuhimiza matumizi ya mifumo bunifu ya ufadhili inayounganisha mitaji kutoka sekta ya umma, sekta binafsi na taasisi za maendeleo ili kupunguza vihatarishi vya uwekezaji, kuongeza upatikanaji wa huduma muhimu na kuweka msingi thabiti wa ukuaji wa uchumi shirikishi. Kwa kushirikiana na taasisi za maendeleo za kimataifa na wadau wa kifedha, Foundation inalenga kuharakisha upatikanaji wa fedha kwa miradi na biashara zinazochochea ajira, kuimarisha uhakika wa chakula na kujenga uchumi imara na endelevu katika maeneo ya vijijini. Ushiriki wa CRDB Bank Foundation katika mkutano huo wa Rome ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya kuchochea maendeleo jumuishi kwa kuunganisha mitaji na fursa zilizopo katika jamii. Wakati majadiliano ya kimataifa kuhusu maendeleo jumuishi na ufadhili endelevu yakiendelea, CRDB Bank Foundation inaendelea kuelekeza nguvu zake katika kubadili ushirikiano kuwa miradi inayotekelezeka, na miradi hiyo kuwa matokeo halisi yanayogusa maisha ya mamilioni ya wananchi wa vijijini nchini Tanzania na kwingineko.
Mon, 05 Oct 2026 09:11:30 +0000J'ai vu près de 500 exécutions, mais jamais une comme celle de Christa Pike
Le journaliste texan Michael Graczyk a vu des exécutions ratées au cours de sa carrière, mais jamais une où un condamné a survécu.
RecentlyMinerals minister orders review of small-scale mining levies
Read the full report from the original source.
RecentlyEndometriosis: Kirinyaga MP urges Government to include treatment under SHA
News · 3 hours ago
RecentlyFood security tops Kenya irrigation agenda, CS Muriithi says
Latest · Business
RecentlyLe candidat d'extrême droite Flávio Bolsonaro remporte le premier tour des élections brésiliennes
Aucun candidat n'ayant obtenu plus de 50 % des voix, un second tour aura lieu le 25 octobre.
RecentlyTwo suspected phone snatchers arrested in Kasarani
Read the full report from the original source.
RecentlyTragedy as boy, 3, drowns in fish pond in Embu
Police said the boy was playing beside the fish pond when he accidentally fell into the water and drowned.
RecentlyPage 874 of 1140 · 22794 stories