Search the region
22767 stories
Audio — Visite du pape Léon XII en France et réforme de l'Église
To play this audio please enable JavaScript, and consider upgrading to a web browser that supports HTML5 video
RecentlyBabu to Sifuna: My brother I support you 100%
Babu said he had supported Sifuna’s presidential ambitions from the beginning.
RecentlyIHG opens 112-suite Voco hotel near JKIA
Latest · Business
RecentlyJambo Jet returns to Uganda after Covid exit
Low-cost carrier Jambo Jet has returned to Uganda, eight years after launching its first international route to Entebbe International Airport. The Kenyan airline first flew…
RecentlyUS Marine arrested over murder of woman in Japan
Japanese Prime Minister Sanae Takaichi described the crime as a "brutal and heinous"
RecentlyEXPENSIVE FIGHT | Highlights pambano la Tano Juma dhidi ya Mganda Tusingwire - 04/10/2026
VITASA | Mtanzania Tano Juma ameshinda kwa pointi dhidi ya Mganda, Joshua Tusingwire.. Pambano la raundi nane. Ni Usiku wa Vitasa Expensive Fight kutoka Golden Tulip, Dar es Salaam. #Vitasa #VitasaNight #ExpensiveFight MafiaBoxing
2026-10-04T16:51:11+00:00BK yahembye aba agent bayo babaye indashyikirwa
Read the full report from the original source.
RecentlyEXPENSIVE FIGHT | Tano Juma amchapa kwa pointi Mganda Tusingwire - 04/10/2026
VITASA | Mtanzania Tano Juma ameshinda kwa pointi dhidi ya Mganda, Joshua Tusingwire.. Pambano la raundi nane. Ni Usiku wa Vitasa Expensive Fight kutoka Golden Tulip, Dar es Salaam. #Vitasa #VitasaNight #ExpensiveFight MafiaBoxing
2026-10-04T16:33:52+00:00AFA Academy, MSF Starlets crowned Safaricom Chapa Dimba Eastern Region champions
Read the full report from the original source.
RecentlyIran airlines resume flights to Iraqi holy city after US exemption
Read the full report from the original source.
RecentlyGrade 7 learner accused of hacking elder brother in dispute over their mother's inheritance
Read the full report from the original source.
RecentlyMAFA Academy, MCF Starlets Crowned Chapa Dimba Eastern Region Champions
football · 4 hours ago
RecentlyChamp Karan ends season with third career ARC title in Tanzania
Latest · Motorsport
RecentlySifuna: Raila may not have reached Canaan, but we will
Sifuna said the circumstances surrounding the registration of the new party made its launch particularly significant
RecentlyMerz pledges military and financial aid on visit to Ukraine
Read the full report from the original source.
RecentlyUS execution survivor critically ill, on ventilator: lawyer
Read the full report from the original source.
RecentlyMAANDALIZI MKUTANO WA 153 IPU YAKAMILIKA, NCHI 159 ZATHIBITISHA USHIRIKI
Na Seif Mangwangi, Michuzi TV Arusha MAANDALIZI ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) yamekamilika jijini Arusha, huku nchi 159 kati ya 183 wanachama wa Umoja huo zikishathibitisha ushiriki wao, katika mkutano unaotarajiwa kuwakutanisha zaidi ya washiriki 2,000 kutoka mabunge mbalimbali duniani. Akizungumza kuhusu maandalizi hayo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio makubwa na kwa kiwango kinacholinda heshima ya taifa. Mkutano huo utafanyika kuanzia Oktoba 5 hadi 9, 2026 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC). Spika Zungu amesema idadi kubwa ya nchi zilizothibitisha ushiriki inaonesha umuhimu wa mkutano huo na fursa ambayo Tanzania imepata ya kujitangaza kimataifa, huku akitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kukubali Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo. Amesema mkutano huo ni fursa muhimu kwa Tanzania, hususan Arusha, kuwaunganisha wageni kutoka nje na wananchi wa ndani, huku akiwataka wakazi wa Arusha kutumia fursa hiyo katika biashara, huduma za malazi, usafiri, utalii na uuzaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini. Spika Zungu amewataka wananchi kutumia ujio wa wageni hao kutangaza bidhaa na fursa zinazopatikana nchini, akitaja bidhaa za asili kama Tanzanite, korosho na bidhaa nyingine, huku akisisitiza umuhimu wa kuonesha ukarimu na kujenga taswira nzuri ya Tanzania kwa wageni watakaorejea katika nchi zao. Kwa upande wake, Balozi Abdallah Posi amesema Mkutano wa 153 wa IPU ni tukio kubwa kwa Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza nchi hiyo kuwa mwenyeji wa mkutano huo unaowakutanisha mabunge kutoka sehemu mbalimbali duniani. Amesema Tanzania imepata nafasi ya kuonesha uwezo wake wa kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa na kuimarisha diplomasia ya kibunge. Balozi Posi amesema wawakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mabunge Duniani na Geneva wana jukumu muhimu la kuiwakilisha na kuitangaza Tanzania katika jumuiya ya kimataifa, na kwamba ofisi hiyo ni kiungo muhimu kati ya Tanzania, Bunge na IPU katika masuala mbalimbali ya kidiplomasia. Aidha, amesema mafanikio ya mkutano huo ni mtihani wa utayari wa Tanzania katika kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, akisisitiza kuwa uwezo wa kufanikisha mkutano unaoshirikisha maelfu ya watu kutoka nchi mbalimbali utaongeza uzoefu na kuifanya Tanzania kuwa na uwezo wa kuandaa matukio mengine makubwa zaidi. Balozi Posi amewataka Watanzania wote, wakiwemo viongozi, wafanyabiashara na waandishi wa habari, kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa zinazotokana na ujio wa wageni hao, akisema wageni watakaa katika hoteli, watatembelea maeneo mbalimbali, watanunua bidhaa na kutumia huduma mbalimbali, hivyo kutoa mchango katika uchumi wa ndani. Amesema fursa hiyo haipaswi kuishia katika diplomasia ya kibunge pekee, bali inapaswa kuzaa matokeo katika sekta ya utalii na biashara, kwani wageni watakaofika Tanzania wanaweza kuwa mabalozi wazuri wa nchi hiyo watakaporejea katika mataifa yao. Spika Zungu amewapongeza Katibu wa Bunge na timu nzima ya maandalizi, pamoja na wahandisi, mafundi, wataalamu na watumishi wengine walioshiriki kuhakikisha miundombinu na huduma muhimu zinakamilishwa kwa ajili ya mkutano huo. Amesema mkutano huo pia ni fursa ya kukuza utalii, kwa kuwa wageni watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali nchini na kujionea utamaduni, mazingira na huduma zinazotolewa na Tanzania. Mkutano huo utajadili masuala mbalimbali ya kimataifa chini ya kaulimbiu inayolenga kuimarisha utawala bora na kuwezesha jamii kupitia ushirikishwaji, imani na fursa kwa wote. Ajenda nyingine zinahusisha amani na usalama, maendeleo endelevu, haki za binadamu, wanawake na vijana pamoja na changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia. Spika Zungu amewataka waandishi wa habari kutumia nafasi yao kuutangaza mkutano huo na kuendelea kuelimisha umma kuhusu fursa zinazopatikana kupitia mkutano huo, akisisitiza kuwa mafanikio yake ni jukumu la Serikali, Bunge, sekta binafsi, wananchi na wadau wengine kwa pamoja. Amesema ujio wa maelfu ya wajumbe kutoka mataifa mbalimbali ni fursa ya Tanzania kuendelea kujenga mahusiano ya kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge, kukuza biashara na utalii, huku Arusha ikiwa mwenyeji wa tukio hilo kubwa la kimataifa na Tanzania ikiweka historia ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani.
Sun, 04 Oct 2026 16:07:34 +0000Global life expectancy bounces back to near pre-pandemic levels, WHO says
Read the full report from the original source.
Recently"Confusion du système immunitaire" : comment des allergies peuvent se développer plus tard dans la vie
On considère souvent les allergies comme le fruit d'une mauvaise pioche durant l'enfance, voire avant la naissance. Pourtant, "n'importe qui peut, à tout moment de sa vie, développer une nouvelle allergie", explique l'al
RecentlyWAZIRI WA ARDHI AENDELEA KUKAGUA MAENEO YA UWEKEZAJI NCHINI
Na Munir Shemweta, WANMM KASULU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, ameendelea na ukaguzi wa maeneo ya uwekezaji ambapo ametembelea eneo la mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la Kasulu Sugar, wilayani Kasulu mkoani Kigoma na kusisitiza umuhimu wa ardhi iliyotolewa kwa uwekezaji kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa. Amesema, Serikali inataka kuona maeneo yote yaliyotolewa kwa wawekezaji yakiendelezwa na kuleta tija kwa mujibu wa makubaliano na mipango iliyowekwa. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndiyo mwenye dhamana ya kuunda Kamati ya Kitaifa ya Kugawa Ardhi ya uwekezaji ambapo mbali na jukumu hilo pia kamati inamshauri Kamishna wa Ardhi katika kushughulikia maombi ya umilikishaji ardhi. Dkt. Akwilapo amefanya ziara hiyo mwishoni mwa wiki katika eneo la mradi huo linalomilikiwa na kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar, lenye ukubwa wa hekta 37,662. Katika ziara hiyo, Dkt Akwilapo alijionea shughuli za uwekezaji zinazofanyika na kutoa msisitizo kwa uongozi wa kampuni kuhakikisha ardhi hiyo inaendelezwa na kutumika kwa shughuli za kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari. "Wizara haitarajii kuona ardhi inayotolewa kwa ajili ya uwekezaji ikiendelea kubaki bila kuendelezwa".amesema Mhe Dkt Akwilapo. Ameupongeza uongozi wa Kasulu Sugar kwa uwekezaji uliofanyika na kuutaka kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili uweze kuchangia uzalishaji wa sukari nchini. "Kuendelezwa kwa eneo hili kutasaidia kuongeza uzalishaji miwa na sukari, kupanua upatikanaji wa bidhaa hiyo sokoni na kuwa na mchango katika kupunguza changamoto ya bei ya sukari nchini". Ameeleza. Ziara hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii iliyotaka maeneo yaliyotolewa kwa shughuli za uwekezaji kukaguliwa kwa lengo la kubaini maeneo yasiyoendelezwa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Mufindi Papers Mills Co. Limited Bw. Satya Narayana amemueleza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa, mradi unaotekelezwa na kampuni yake unatumia teknolojia ya hali ya juu na ya kisasa katika uzalishaji sukari. "Mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari katika kiwanda hiki unagharimu dola 320 milioni na unatarajia kuchangia uchumi wa Tanzania na jamii kwa ujumla". Amesma. Eneo la mradi wa Kasulu Sugar wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma linahusisha vijiji saba vya Nyarugusu, Kiyungwe, Kitanga, Kamtundu, Nyamidaho, Kigadye na Heru Ushingo, vilivyotoa ardhi kwa ajili ya uwekezaji wa mradi huo. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea na jitihada za kufuatilia matumizi ya ardhi kwenye maeneo ya uwekezaji kwa lengo la kuhakikisha rasilimali hiyo inatumika kwa tija, kwa kuzingatia mipango ya matumizi ya ardhi na masharti yaliyowekwa. Hatua hiyo inalenga kuimarisha usimamizi wa ardhi, kuhakikisha wawekezaji wanatimiza wajibu wao na kuongeza mchango wa uwekezaji katika kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akioneshwa sehemu ya eneo la uwekezaji kutoka kwa Meneja Mradi wa eneo la uwekezaji kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar Bw. Niket Pande wakati wa ziara ya kutembelea eneo la mradi huo wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma mwishoni mwa wiki. Wa pili kulia ni mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini Mhe. Edibily Kazala Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akipata maelezo kutoka kwa Meneja Usalama, Afya na Mazingira wa kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar Bw. Ahned Shaban (Kushoto) wakati alipotembelea eneo la mradi huo wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma mwishoni mwa wiki. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha sukari cha Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Satya Vekanta (wa pili kulia) alipotembelea eneo hilo la uwekezaji wilayani Kasulu mkoa wa Kigoma mwishoni nwa wiki. Wa pili kushoto ni mbunge wa jimbo la Kasulu Vijijini Mhe. Edibily Kazala. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea eneo la uwekezaji mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar tarehe 2 Oktoba 2026. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akingumza na uongozi wa kampuni ya uwekezaji mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji Sukari wa kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar alipofanya ziara kwenye eneo la mradi huo wilayani Kasulu mkoani Kigoma tarehe 2 Oktoba 2026. Meneja Mradi eneo la uwekezaji kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la kampuni ya kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar tarehe 2 Oktoba 2026. Bw. Niket Pande akielezea namna mradi wa kiwanda cha sukari unavyofanyika wakati wa ziara ya Waziri wa ardhi tarehe 2 Oktoba 2026 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Akwilapo akitembelea moja ya maeneo ya uwekezaji mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la kampuni ya kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar mwishoni mwa wiki. Meneja Mradi eneo la uwekezaji kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la Kasulu Sugar Bw. Niket Pande (kushoto) akimuelezea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo namna pampu ya maji inavyofanya kazi wakati alipotembelea eneo hilo la uwekezaji wilayani Kasulu mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited Bw. Satya Narayana. Munonekano wa eneo la shamba la miwa katika eneo la uwekezaji mradi wa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari la kampuni ya kampuni ya Mufindi Papers Mills Co. Limited, maarufu kama Kasulu Sugar. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)
Sun, 04 Oct 2026 16:02:08 +0000Page 884 of 1139 · 22767 stories