Unganishwa

Search the region

22762 stories

Uncategorized · HabariLeo

IPU yaibua fursa bidhaa za asili

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · DW Rwanda

Trump names AI czar to head White House task force

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Edwin Sifuna unveils his new party, The Equitable Party

Read the full report from the original source.

Recently
National · HabariLeo

Serikali yasisitiza mageuzi madini Dira 2050

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

KUMEKUCHA !MISS DARZONE KUONDOKA NA GARI MPYA

MASHINDANO Ya Urembo Miss Dar zone yachukua sura mpya baada ya kuita Warembo 12 tu kutoka katika mashindano ya wilaya za Dar es Salaam . Akizungumza na Michuzi  Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio Maarufu Kama Mama J'adore amesema kutokana na uzoefu wake wakuandaa mashindano mbalimbali huku akijinasibu kuwa warembo wengi wamepita katika mikono yake huku akitoa Miss Tanzania ambae amefanya vizuri hadi kufikia Miss World Sylvia buberwa ,hivyo kuhaidi kupitia mashindano hayo ya Miss Darzone wategemee Miss Tanzania atapatikana kutoka hapo. "Mwaka huu tunatarajia kuwa na msimu mkubwa zaidi, wenye ushindani, burudani na matukio mbalimbali yatakayotufikisha kwenye kilele cha safari hii ya Miss Darzone ambapo tutachukua Warembo 12 tu katika mashindano madogo ya mkoa wa Dar es Salaam ambapo kwa sasa tunasubiri mchakato wa kupatiwa kwao." Muandaaji huyo ameongeza kuwa  warembo wataingia kambini mwezi Oktoba huku  kilele chake Novemba 12,2026 ambapo zawadi kwa atakaevikwa taji ataondoka na gari mpya ambayo itawekwa wazi hivi karibuni aina ya gari hiyo na thamani yake. Pia amewaomba Wazazi na Walezi kuwaruhusu mabinti zao  kushiriki mashindano hayo ya Urembo kwani Urembo sio uhuni kama inavyotafsiriwa na baadhi ya watu badala yake Mashindano hayo yamekuwa yakitoa Wasichana ambao wamekuwa mfano wa kuigwa ,Viongozi wa Kitaifa na Wasaidizi wa Jamii zao. Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio Maarufu Kama Mama J'adore akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza rasmi ufunguzi wa Shindano hilo huku akiwasisitiza Wazazi kuwaruhusu mabinti kushiriki katika shindano hilo Picha ya Pamoja Muandaaji wa shindano la Miss Dar zone Ruth Urio akiwa na Wadhamini pamoja na Mawakala wa Mashindano ya Urembo kutoka Wilaya za Jijini Dar es Salaam

Sun, 04 Oct 2026 13:49:26 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

Leaders rally behind Sifuna as he unveils new party

The leaders, who attended the launch, urged Sifuna to build the party into a national outfit

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

Vodacom Coastal Classic Yaunganisha Michezo, Utalii na Maendeleo ya Vijana Africa

Mkurugenzi wa Vodacom Business wa Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic upande wa wanawake, Mary Aleper (katikati) kutoka Uganda. Washindi wengine wa mashindano hayo walikuwa Ditona Munu Martinie mshindi wa pili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) (wa pili kushoto) na Mercy Elegae kutoka Kenya, aliyeshika nafasi ya tatu. Washindani wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic wakiwa katika eneo la kuanzia mashindano hayo kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, kuelekea Bagamoyo, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Tehama wa Vodacom Tanzania Plc Athumani Mlinga Mshindi wa Kwanza wa Mashindano ya Vodacom Coastal Classic upande wa wanaume Charles Kagimu kutoka Uganda (katikati) mshindi wa pili Jordan Schleck kutoka Uganda (kushoto) na mshindi wa tatu Boniphace Ngwata kutoka Tanzania (kulia), wakionesha mfano wa hundi walizokabidhiwa katika mashindano hayo. Washindi hao walijishindia milioni 10 kwa mshindi wa kwanza, milioni 7 kwa mshindi wa pili, na milioni 5 kwa mshindi wa tatu mtawalia. Washiriki wa Mashindano ya Nyerere Cycling Tour wakiendelea na Mashindano hayo ukanda wa Pwani wa bahari ya Hindi kuelekea Bagamoyo Mkurugenzi wa Vodacom Business kutoka Vodacom Tanzania PLC Nguvu Kamando (kulia), na mwanzilishi wa msafara wa baiskeli wa Nyerere Cyling Tour Gabriel Landa kushoto, wakiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa mashindano wa Cycling Tour Upande wa wanawake, Mary Aleper kutoka Uganda aliyeshika nafasi ya kwanza (katikati), Ditona Munu Martinie kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyeshika nafasi ya pili (wa pili kushoto), na Mercy Elegae kutoka Kenya aliyeshika nafasi ya tatu (wa pili kulia). Washindi hao walijishindia kiasi cha shilingi milioni 10, milioni saba na milioni tano kila mmoja. ========. ========. ========. ========== Vodacom Coastal Classic Yaunganisha Michezo, Utalii na Maendeleo ya Vijana Africa Bagamoyo, Pwani - 4 Oktoba 2026: Uzinduzi wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic umeonesha namna ambavyo michezo inaweza kuwa chachu ya kukuza utalii, elimu na maendeleo ya jamii, huku mashindano hayo ya kuendesha baiskeli yakitoa fursa ya kuonesha vivutio vya utalii vilivyopo katika ukanda wa pwani ya Tanzania na kuunga mkono shughuli zenye manufaa ya muda mrefu kwa jamii ambazo msafara wa waendesha baiskeli wa Nyerere Cycling Tour (zamani Twende Butiama) utapita. Kwa kuwakutanisha waendesha baiskeli, jamii na wadau mbalimbali, mashindano hayo yametoa mchango katika kukuza utalii wa ndani, kuhamasisha vijana kupitia michezo na kusaidia jitihada za elimu na maendeleo katika maeneo yanayounganishwa na safari hiyo. Mashindano hayo, ambayo ni sehemu ya maandalizi kuelekea msafara wa Nyerere Cycling Tour, yaliwakutanisha waendesha baiskeli 147 walioshiriki mbio hizo zilizopita katika maeneo ya kuvutia ya ukanda wa pwani ya Tanzania. Mbali na kutoa ushindani kwa waendesha baiskeli, mashindano hayo yameendelea kuonesha fursa za utalii nchini na kuongeza uelewa kuhusu shughuli za elimu, afya na uhifadhi wa mazingira zitakazotekelezwa katika maeneo mbalimbali wakati wa safari ya msafara huo kuelekea Butiama. Afisa Mwandamizi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Charles Maguzu aliwapongeza waandaaji na washiriki wa mashindano hayo kwa kutumia michezo kama jukwaa la kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi, huku ikiendelea kuimarisha nafasi ya Tanzania kama kituo cha utalii wa michezo. “Vodacom Coastal Classic ni ushahidi wa namna mchezo wa baiskeli unavyozidi kuwa na nafasi muhimu katika kuhamasisha maisha yenye afya, kutoa fursa kwa vijana wenye vipaji na kuonesha vivutio vya utalii vya Tanzania. Kupitia matukio kama haya, hatuendelezi vipaji vya michezo pekee, bali pia tunachangia katika elimu, uelewa kuhusu uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya jamii. Tunawapongeza Vodacom na washirika wote kwa kuendelea kuwekeza katika kukuza mchezo huu na kuhamasisha kizazi kijacho cha waendesha baiskeli,” alisema. Baada ya ushindani mkali, Charles Kagimu Kutoka Uganda na Mary Aleper kutoka Uganda waliibuka washindi wa mashindano ya Vodacom Coastal Classic 2026 baada ya kumaliza katika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanaume na wanawake, ambapo kila mmoja alizawadiwa shilingi milioni 10. Mashindano hayo yaliwapa waendesha baiskeli fursa ya kutumia vipaji vyao kama chanzo cha kipato kupitia ushindani wa kitaaluma, huku yakihamasisha vijana zaidi kushiriki katika mchezo huo. Washindi wa nafasi ya kwanza katika kila kundi walipata shilingi milioni 10, huku washindi wa nafasi ya pili wakipata shilingi milioni 7 na nafasi ya tatu shilingi milioni 5. Waendesha baiskeli waliomaliza katika nafasi ya nne hadi ya kumi katika kila kundi walizawadiwa shilingi milioni 1 kila mmoja. Akizungumza baada ya mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business wa Vodacom Tanzania PLC Nguvu Kamando, aliwapongeza washindi pamoja na waendesha baiskeli wote walioshiriki, akieleza kuwa mashindano ya Vodacom Coastal Classic yataendelea kutoa fursa kwa waendesha baiskeli kuonesha vipaji vyao huku yakichangia katika malengo mapana ya maendeleo ya taifa. “Zaidi ya ushindani wenyewe, Vodacom Coastal Classic na Nyerere Cycling Tour zinasaidia kukuza utalii wa ndani, kuunga mkono shughuli za elimu na kuhamasisha matokeo chanya ya kijamii katika jamii zinazopitiwa na safari hii. Tunajivunia kuwa sehemu ya jukwaa linalowawezesha vijana, wakiwemo wasichana, huku likitumia michezo kama nyenzo ya kuchochea maendeleo,” alisema. Kwa upande wake, Meneja wa Uendelevu wa Stanbic Bank Tanzania, Annette Nkini, alisema ushirikiano huo unaonesha dhamira ya benki hiyo katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi hapa nchini. “Kwa miaka 30, Tanzania imekuwa zaidi ya soko kwa Stanbic Bank; ni nyumbani kwetu. Vodacom Coastal Classic na Nyerere Cycling Tour vinaonesha uwezo wa Tanzania katika utalii, vinawekeza katika elimu na vinafungua fursa kwa vijana na jamii kustawi. Kupitia ushirikiano huu tunawekeza kwa watu na jamii ambao maendeleo yao yataendelea kuijenga Tanzania ya kesho," alisema. Aliongeza kuwa Stanbic Bank itaendelea kuunga mkono mashindano hayo kupitia ushirikiano wake katika Nyerere Cycling Tour na jitihada za kuhamasisha Watanzania wengi zaidi kushiriki mchezo wa baiskeli kama fursa ya michezo na uchumi.Vodacom Coastal Classic ni sehemu ya shughuli zinazoambatana na Nyerere Cycling Tour, ambayo itahusisha safari ya kilomita 1,500 kutoka Dar es Salaam hadi Butiama kuanzia tarehe 5 hadi 14 Oktoba 2026. Safari hiyo itawakutanisha waendesha baiskeli kutoka Tanzania na nchi nyingine, sambamba na shughuli zinazolenga kuhamasisha elimu, afya na uhifadhi wa mazingira katika maeneo mbalimbali yatakayopitiwa. Kampuni ya Vodacom Tanzania ndyo mshirika mkuu wa Nyerere Cycling Tour, huku Afro Oil, Stanbic Bank Tanzania, BYD, ABC, Coca-Cola na Huawei zikiwa miongoni mwa washirika wanaounga mkono mpango huo kwa ujumla. Kumalizika kwa mashindano ya Vodacom Coastal Classic sasa kunaweka msingi wa kuendelea kwa safari ya Nyerere Cycling Tour, huku waendesha baiskeli wakijiandaa kuendelea na safari kuelekea Butiama, nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Sun, 04 Oct 2026 08:30:00 +0000
Uncategorized · Mwananchi

Mwabukusi aiburuta Kamati ya Mawakili mahakamani

Soma zaidi...

Recently
Uncategorized · KT Press

Ruberwa: Kabila Acted Against Banyamulenge Killings, Tshisekedi Ignored My 15 Appeals

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

MPs test out digital number plate tracking system

Parliament’s committee on Physical Infrastructure says it has established that the digital number plate system can effectively track vehicles. Led by committee chairperson Mwine Mpaka,…

Recently
Uncategorized · The Citizen

Chivayo and Ginimbi: The tale of two African billionaires whose lives were tragically cut short

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Daily News

Tanzania bolsters reforms in mining sector in line with its Vision 2050 goals

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

PSSSF-HAKIKINI TAARIFA ZENU ILI "MLIPWE JANA"

Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Thomas Labi akitoa huduma kwa mwanachama wakati wa maonyesho ya 9 ya Technologia ya madini mkoani Geita. Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo (kushoto), akikabidhi zawadi kwa kaimu Katibu tawala Mkoa wa Geita Bw. Charles Chacha siku ya mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Kaimu Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Nathan Makuchilo, akitoa huduma ya elimu na huduma za PSSSF alipotembelea banda la Benk Kuu ya Tanzania alipofanya ziara ya banda kwa banda Maafisa wa PSSSF wakitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF walipofanya ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la Benk kuu ya Tanzania Afisa wa PSSSF akitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF wakati wa ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la Bima ya Afya. Maafisa wa PSSSF wakitoa huduma na elimu kuhusu bidhaa za Mfuko wa PSSSF walipofanya ziara ya banda kwa banda walipotembelea banda la mahakama kuu ya Tanzania Geita, Oktoba 3, 2026 Meneja wa PSSSF kanda ya Ziwa Magharibu, Bw.Thomas Labi, amewasihi wastaafu tarajiwa kuhakiki taarifa zao mapema kabla ya siku ya kustaafu, ili kuhakikisha wanalipwa jana kwa wakati na usahihi. Bw. Labi amesema hayo katika Maonyesho ya Tisa ya Teknolojia ya Madini Mkoani Geita, ambayo yamehitimishwa Oktoba 3 2026, baada ya kudumu kwa siku 11, ambapo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekamilisha utoaji wa elimu na huduma kwa wananchi, watumishi wa umma, na wastaafu watarajiwa kupitia banda lake. “Mfuko unadhamiria kuhakikisha makundi yote yanapata huduma na elimu kwa uelewa sahihi, tunashukuru watumishi wapya waliotembelea banda la PSSSF na kupata elimu juu ya PSSSF, Hifadhi ya Jamiii na elimu ya matumizi ya huduma za kidigitali”alifafanua Bw. Labi. Katika maonesho hayo, PSSSF ilitoa elimu ndani ya banda, timu ya PSSSF ikiongozwa na Kaimu Meneja Bw. Nathan Makuchilo, pia imetembelea wanachama moja kwa moja kwenye mabanda yao (banda kwa banda) ili kuendelea kuwafahamisha na kuwahudumia kwa njia ya kidigitali. Wanachama waliotembelea banda la PSSSF wameonyesha kuridhishwa na huduma walizopata, hasa matumizi ya mfumo wa PSSSF Member Portal unaowawezesha kuangalia taarifa zao kupitia simu za mkononi. Pamoja na kufungwa kwa maonyesho hayo, Bw. Thomas Labi ametoa wito kwa wanachama na wananchi wote kuendelea kutembelea Ofisi za PSSSF zilizopo kote nchini ili kupata ufumbuzi wa changamoto, kuwasilisha kero au malalamiko, na kupata majibu kuhusu huduma za Mfuko.

Sun, 04 Oct 2026 13:15:33 +0000
Uncategorized · Daily News

Tanzania orders residents living in high-risk areas of Msimbazi River to relocate before El Nino rains

DAR ES SALAAM: THE Minister of State in the Vice-President’s Office (Union and Environment), Hamad Yussuf Masauni, has urged residents…

Recently
Uncategorized · The Standard

Sifuna unveils Equitable Party, as leaders promise to unite Kenyans

Nairobi Senator Edwin Sifuna has unveiled Equitable Party as his political vehicle for the 2027 General Election.

Sun, 04 Oct 2026 15:51:05 +0300
Uncategorized · Citizen Digital

England healing pain of World Cup heartache says Tuchel

Read the full report from the original source.

Recently
Health · Daily News

Tanzania’s global workforce is growing, but is employee health insurance ready for international mobility?

DAR ES SALAAM: For years, conversations with employers in Tanzania about medical insurance have centred on familiar questions: Which hospitals…

Recently
National · Issa Michuzi

MCHENGERWA AUNGURUMA, AWAPIGA TAFU YA MIL.35 WANAWAKE WA UWT PWANI

Na Victor Masangu, Pwani WAZIRI wa Afya, Mohamed Mchengerwa, ametoa Sh milioni 35.1 kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani, ikiwa ni sehemu ya kuwaunga mkono katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba za makatibu wa jumuiya hiyo katika ngazi ya Mkoa na Wilaya. Mchengerwa, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), ametoa mchango huo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kikao cha Baraza la Kawaida la UWT Mkoa wa Pwani, kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wa chama na Serikali, wakiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo. Akizungumza katika kikao hicho, Mchengerwa alisema ameamua kutoa mchango huo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuwawezesha wanawake kiuchumi na kuimarisha jumuiya zao. Alisema ataendelea kushirikiana na wanawake wa UWT kwa hali na mali, hususan katika kuwawezesha kutekeleza miradi ya maendeleo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kupunguza utegemezi. “Nimefarijika sana kualikwa katika kikao hiki cha Baraza la Kawaida la UWT Mkoa wa Pwani. Nimechangia Sh milioni 35.1 kwa ajili ya kuwasaidia wanawake katika mambo mbalimbali, ikiwemo miradi ya ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi za Wilaya na Mkoa,” alisema Mchengerwa. Alisema anatamani kuona wanawake wakijenga uwezo wa kiuchumi na kuwa na miradi endelevu itakayowasaidia wao pamoja na jumuiya kwa ujumla. Mchengerwa pia aliwahimiza wanawake wa Pwani kudumisha umoja, mshikamano na amani, akiwataka kuachana na tabia zinazoweza kuvuruga mshikamano wao na badala yake kuweka misingi imara ya kuimarisha jumuiya na chama. MARIAM AKABIDHI PIKIPIKI 10 Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahimu, amekabidhi pikipiki 10 kwa UWT Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kuwaingizia kipato. Mariam alisema ametumia sehemu ya fedha za mshahara wake kusaidia kuwawezesha wanawake kiuchumi, ambapo pikipiki hizo zitatumika kama kitega uchumi katika jumuiya hiyo. Alisema pikipiki hizo zitatumika katika ngazi mbalimbali za UWT, huku akisisitiza kuwa lengo ni kuwawezesha wanawake kuanzisha miradi itakayowasaidia kujitegemea na kuondokana na utegemezi. “Nimeamua kutumia fedha zangu za mshahara kwa ajili ya kuwasaidia wanawake wa Mkoa wa Pwani. Nimekabidhi pikipiki 10 ambazo zitasaidia jumuiya za wanawake katika Wilaya mbalimbali na kuwawezesha kujikwamua kiuchumi,” alisema Mariam. Mbali na pikipiki hizo, Mariam pia alikabidhi vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kusaidia utekelezaji wa miradi ya ujenzi ya UWT Mkoa wa Pwani. UWT YAPANIA KUJITEGEMEA Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani, Zainabu Vullu, alisema jumuiya hiyo imeweka mikakati ya kuondokana na utegemezi kwa kuanzisha na kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo yenye tija kwa wanawake. Alisema lengo ni kuhakikisha UWT inakuwa na miradi endelevu itakayowezesha jumuiya hiyo kujiendesha na wakati huo huo kuwasaidia wanawake kiuchumi. Naye Katibu wa UWT Mkoa wa Pwani, Aziza Omary, alisema wamejiandaa kutekeleza mipango mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi ya Mkoa na Wilaya. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, aliwataka wanawake kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali, ikiwemo mikopo ya asilimia 10 inayotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi. Alisema wanawake wanapaswa kutumia fursa hizo kuanzisha na kuendeleza miradi yenye tija badala ya kuendelea kuwa tegemezi. Katika kikao hicho, wajumbe walijadili masuala mbalimbali, ikiwemo uanzishwaji na uendelezaji wa miradi ya maendeleo, ujenzi wa nyumba za makatibu wa UWT katika ngazi ya Mkoa na Wilaya, mikakati ya kuimarisha jumuiya na uhai wa wanachama, pamoja na namna bora ya kutumia pikipiki walizopewa kama vitega uchumi.

Sun, 04 Oct 2026 13:08:24 +0000
Uncategorized · The Star Kenya

[PHOTOS] Sifuna unveils his political party

Sifuna has been unveiled as TEP party leader during an event in Nairobi Sunday

Recently
Uncategorized · Daily News

NBC reinforces tourism growth commitment through Arusha engagement

ARUSHA: National Bank of Commerce (NBC) is expanding its focus on Tanzania’s tourism sector, citing growing demand for financing and…

Recently

Page 886 of 1139 · 22762 stories