Search the region
22740 stories
Viongozi wa dini Kimara wapewa msaada wa vyakula
Read the full report from the original source.
RecentlyInside Kenya’s maternal health gap, the fight to save mothers and newborns
Read the full report from the original source.
RecentlyBosnia-Herzegovina shaped by war, separatism, EU ambitions
Read the full report from the original source.
RecentlyIs Gen. Salim Saleh The Solution to Uganda’s Succession Dilemma?
By Agaba Muzoora “A prospective leader is judged not only by what he promises to do with power, but also…
Recently“I am Not Willing to Defend Corrupt RDCs,” Says Minister Babalanda as “Expose the Corrupt Campaign” Intensifies
The Minister for the Presidency, Hon. Babirye Milly Babalanda, has said her office will not shield or defend Resident District Commissioners (RDCs) implicated in corruption, as the Government intensifies its…
Recently“This Fight Is Bigger Than Money”: Sudhir Ruparelia Speaks Out on £300M London Crane Bank Lawsuit
KAMPALA / LONDON — Tycoon Sudhir Ruparelia has broken his silence on the ongoing £300 million (about UGX 1.4 trillion) legal battle in the London High Court involving the Bank…
RecentlyOpposition Gives Ruto 14 Days to Release Dangote-Lamu Refinery Deal
Latest · Investments in Africa
RecentlyBURIANI DKT. KAVURA: TPSC YAMUENZI KWA MCHANGO WAKE KATIKA MAENDELEO YA CHUO NA UTUMISHI WA UMMA
Na Shakiru Abdulkarim Uhai wa mwanadamu una mwisho, lakini mchango wake katika maisha ya wengine unaweza kuendelea kuishi kwa vizazi. Kifo cha Dkt. Richard Mwenyewe Kavura, kilichotokea tarehe 2 Oktoba 2026 nyumbani kwake Goigi, Mbezi Beach, Dar es Salaam, kimeacha pengo katika jumuiya ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC), huku kikitukumbusha thamani ya urithi aliouacha. Akiwa Mkuu wa kwanza wa Chuo kuanzia mwaka 2000 hadi 2005, alikiongoza katika miaka yake ya mwanzo na kushiriki kuweka misingi ya mafunzo, tafiti na ushauri wa kitaalamu kwa ajili ya kuendeleza utumishi wa umma. “Tunamkumbuka Dkt. Kavura kwa kuweka misingi muhimu ya maendeleo ya Chuo chetu. Uongozi wake katika miaka ya mwanzo uliunganisha mafunzo na mahitaji ya utumishi wa umma, na mchango huo utaendelea kuwa sehemu ya historia ya TPSC.” — Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho. Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania kimetimiza miaka 25 tangu kuanzishwa kwake. Katika sherehe za kilele cha Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chuo, zilizofanyika tarehe 3 Julai 2026 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, TPSC ilitambua mchango wa Dkt. Kavura na kumtunuku tuzo kwa mchango wake katika maendeleo ya Chuo. KUMBUKUMBU : Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. Ridhiwani Jakaya Kikwete, akimkabidhi Dkt. Richard Mwenyewe Kavura tuzo ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya TPSC, wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Miaka 25 ya Chuo, tarehe 3 Julai 2026, jijini Dar es Salaam. Dkt. Kavura alizaliwa tarehe 22 Agosti 1944. Alipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Kakonko, wilayani Kibondo- Kigoma, na baadaye akasoma katika Shule ya Sekondari St. Mary’s, Tabora, na Shule ya Sekondari Shinyanga. Mwaka 1970, alihitimu Shahada ya Sanaa katika Elimu kutoka Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki, Dar es Salaam. Alipata Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Windsor, Canada, mwaka 1975, na Shahada ya Uzamivu katika Usimamizi kutoka Chuo Kikuu cha Cranfield, Uingereza, mwaka 1983. Safari yake ya kulitumikia taifa kupitia elimu ilianza mwaka 1970 akiwa mwalimu katika Shule ya Sekondari Lindi, ambako alifundisha hadi mwaka 1971. Baadaye, alifundisha katika Shule ya Sekondari Shinyanga kuanzia mwaka 1971 hadi 1972. Katika kipindi hicho, alifundisha masomo ya Kiingereza, Historia na Jiografia. Kuanzia mwaka 1972 hadi 1988, alifanya kazi katika iliyokuwa Taasisi ya Maendeleo ya Uongozi (IDM), Mzumbe, akiwa mhadhiri na baadaye mhadhiri mwandamizi. Alifundisha masomo ya masoko, utafiti wa masoko na usimamizi wa mauzo, pamoja na kushiriki katika programu za kuwajengea uwezo viongozi wa ngazi za juu. Aidha, aliongoza Idara ya Mafunzo ya Biashara na kufanya tafiti na kazi za ushauri katika masoko, rasilimali watu, mahitaji ya mafunzo na usimamizi wa taasisi. Utumishi wake katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ulimpa nafasi nyingine ya kuchangia maendeleo ya elimu ya juu nchini. Alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo kuanzia mwaka 1988 hadi 1991, na Mkuu wa Chuo kuanzia mwaka 1991 hadi 1995. Mafanikio katika kipindi cha uongozi wake IFM yalihusisha kuongezeka kwa udahili kutoka takribani wanafunzi 600 hadi zaidi ya 1,000 na kuongezeka kwa idadi ya wahadhiri kutoka takribani 30 hadi 50. Pia, sifa za kitaaluma za wahadhiri ziliendelezwa kupitia masomo ya uzamili na uzamivu. Alichangia kuanzishwa kwa programu mpya za kitaalamu, zikiwemo za teknolojia ya habari, pamoja na kuboresha miundombinu na vifaa vya kufundishia. Kuanzia mwaka 1995 hadi 1998, kupitia Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Dkt. Kavura alikuwa Mshauri Mkuu wa Kiufundi katika Taasisi ya Utawala wa Umma ya Lesotho (LIPAM). Katika nafasi hiyo, alishiriki katika kuimarisha usimamizi wa taasisi, mitaala, uwezo wa wakufunzi, miundombinu na shughuli za tafiti na ushauri. Mwaka 1999 hadi 2000, alirejea IFM akiwa Mkurugenzi wa Shule ya Mafunzo ya Uzamili na Kituo cha Utafiti. Alisimamia maendeleo ya mafunzo ya uzamili, tafiti, machapisho na ushauri wa kitaalamu, pamoja na viwango vya ubora katika shughuli za kitaaluma. Uzoefu huo ulikuwa msingi muhimu wa kuiongoza TPSC. Alipokuwa Mkuu wa kwanza wa Chuo mwaka 2000, alisimamia shughuli za mafunzo, tafiti na ushauri wa kitaalamu, huku akiongoza maboresho yaliyolenga kukiwezesha Chuo kukidhi mahitaji ya watumishi wa umma. Katika kipindi chake cha uongozi, majengo na maeneo ya kufundishia yalifanyiwa ukarabati na upanuzi. Madarasa na ofisi ziliongezewa samani, na Chuo kikapata vifaa vya kazi na kujifunzia, vikiwemo kompyuta, vitabu na vifaa vya mafunzo. Mchango mwingine muhimu ulikuwa kuelekeza mitaala katika mahitaji ya Programu ya Mageuzi ya Utumishi wa Umma. Chuo kilianzisha mafunzo katika uongozi, usimamizi, utawala na usimamizi wa kumbukumbu. Idadi ya waliojiunga na mafunzo iliongezeka kutoka 2,166 mwaka 2000/2001 hadi 5,195 mwaka 2004/2005. Mapato yatokanayo na shughuli kuu za Chuo nayo yaliongezeka kutoka shilingi milioni 753 hadi shilingi bilioni 2.1 katika miaka hiyo. Mbali na uongozi wa taasisi, Dkt. Kavura alishiriki katika kuandaa na kutoa mafunzo, kutathmini mahitaji ya mafunzo na kuandaa mipango ya maendeleo ya watumishi. Maeneo aliyoyafanyia kazi yalijumuisha uongozi, utawala bora, mipango ya kimkakati, usimamizi wa utendaji na rasilimali watu. Wasifu wake unaeleza ushiriki wake katika programu za mafunzo kwa wakuu wa wilaya, watumishi wa sekretarieti za mikoa na watumishi wa Ikulu. Baada ya kustaafu TPSC, aliendelea kulitumikia taifa kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kuanzia mwaka 2006 hadi 2010, alikuwa mtaalamu wa kujenga uwezo wa watumishi kupitia Programu ya Mageuzi ya Utumishi wa Umma. Majukumu yake yalihusisha kuendeleza sera na mikakati ya kujenga uwezo katika wizara, idara na wakala za Serikali, kushiriki katika kuandaa sera ya mafunzo kwa utumishi wa umma, na kusaidia uandaaji wa mipango ya maendeleo ya rasilimali watu. Aidha, alichangia uongozi katika elimu kupitia ushiriki katika bodi na mabaraza ya taasisi, zikiwemo Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, IDM Mzumbe, Chuo cha Elimu ya Biashara na Taasisi ya Uhasibu Arusha. “Kumuenzi Dkt. Kavura ni kuendeleza misingi aliyoiweka katika kukijenga Chuo chetu. Tutaendelea kutoa mafunzo yenye ubora, kufanya tafiti zinazojibu mahitaji ya utumishi wa umma na kutoa ushauri wa kitaalamu unaoboresha utendaji katika Utumishi wa Umma. Heshima ya kudumu kwake itaonekana katika uwezo wa Chuo kuwajengea watumishi maarifa na ujuzi unaowawezesha kutoa huduma bora kwa wananchi,” amesema Mkuu wa Chuo na Mtendaji Mkuu, Dkt. Ernest Mabonesho. Buriani, Dkt. Richard Mwenyewe Kavura. Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi. Amina .
Sat, 03 Oct 2026 19:08:48 +0000Narok: Police shoot one dead as clashes erupt over mining site eviction
Read the full report from the original source.
RecentlyLes violences entravent la riposte contre Ebola en Ituri
Read the full report from the original source.
RecentlyNdejembi: Ni wakati wa utekelezaji fursa zilizopo Afrika
Read the full report from the original source.
RecentlyDaphrose Gauthier du CPCR est décédée Samedi 03 Octobre 2026 à l’âge de 72 ans
Read the full report from the original source.
RecentlyDefence College of Health Sciences officially opens at Gako
Read the full report from the original source.
RecentlySerengeti Lite Nyota Bigi Msimu wa Pili Yawakutanisha Vijana Dar es Salaam
Dar es Salaam iliwaka wakati vijana wenye vipaji mbalimbali walipokutana katika usaili wa Serengeti Lite Nyota Bigi Msimu wa Pili, wakipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kung’arisha vipaji walivyonavyo. Usaili huo umeleta pamoja vijana wenye vipaji vya kuimba, kucheza, kuigiza, kuchekesha, wanamitindo na ubunifu mwingine mbalimbali, na kuwaleta kwenye jukwaa moja ili waonyeshe kile wanachoweza kufanya mbele ya watazamaji na wataalamu wa tasnia. Kupitia ushirikiano na KUNTA Africa, Serengeti Lite inaendelea kutoa nafasi kwa vijana kuamini vipaji vyao, kuvitumia na kufikiria zaidi kupitia kaulimbiu “Lite Your Imagination.” Baada ya Dar es Salaam, safari ya kutafuta Nyota Bigi inaendelea Arusha, Dodoma na Mwanza, ambapo vijana wengine watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi ya kuwa Nyota Bigi wa msimu huu. Nani ataibuka kuwa Nyota Bigi? Safari bado inaendelea.
Sat, 03 Oct 2026 09:30:00 +0000Uhuru hits back at Ruto over attacks, political criticism
Latest · CHURCH & POLITICS
RecentlyLamu residents ask gov't for alternative land as Dangote refinery project takes shape
Read the full report from the original source.
RecentlyWarembo walioandikiwa nyimbo na Barnaba
MBALI na uimbaji wake wa kuvutia, sifa nyingine kubwa ya Barnaba ni kujua kuandika nyimbo vizuri na amewaandikia wanamuziki wenzake wengi.
RecentlyNGAO YA JAMII 2026 | Simba Queens 1-0 JKT Queens | Highlights - 03/10/2026
#NgaoYaJamiiWanawake: Tazama namna Aisha Mnunka wa Simba Queens alivyochomoka kama mshale na kwenda ‘kuwatungua’ JKT Queens. Hili ndilo goli lililoipa ushindi wa Ngao ya Jamii Simba Queens. FT: Simba Queens 1-0 JKT Queens #KariakooDerbyWanawake #NgaoYaJamii2026 #Wanawake #TFF #Fainali #SimbaQueens #JKTQueens #SimbaQueensJKTQueens
2026-10-03T18:35:49+00:00Tennessee prison chief quits over aborted execution
Read the full report from the original source.
RecentlyCHONGOLO ATETA NA WADAU WA TUMBAKU KUTATUA CHANGAMOTO
WAZIRI wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amefanya mkutano na Wadau wa Tasnia ya Tumbaku mkoani Tabora tarehe 3 Oktoba 2026 kutatuai changamoto za tasnia hiyo kuanzia ya bei ya pembejeo, masoko, teknolojia duni ya ukaushaji pamoja na madeni ya AMCOS na halmashauri ambayo hayajalipwa kwa wakati. Kikao hicho kimewahusisha wakulima; Vyama vya Msingi (AMCOS); wanunuzi pamoja na Bodi ya Tumbaku Tanzania; ambapo Mhe. Chongolo amezitaka kampuni zinazodaiwa fedha za wakulima kuhakikisha malipo yote yamekamilika ifikapo tarehe 30 Oktoba 2026, akisisitiza kuwa hakuna sababu ya kuchelewesha malipo baada ya wakulima kuuza Tumbaku. Kuhusu bei ya pembejeo, Mhe. Chongolo amesema Serikali imechelewesha kutangaza bei kwa makusudi ili kutafuta unafuu kwa wakulima. Ameelekeza kufanyika mazungumzo ya wadau ndani ya siku kumi (10) ili kupata bei nafuu zaidi, huku akisisitiza kuwa mbolea lazima isambazwe kwa wakulima ndani ya wiki mbili. Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Dkt. Gerald Mongella, amesema kuwa uchumi wa mkoa huo unategemea zao la Tumbaku huku akisisiriza Serikali kuongeza kiwango cha ruzuku kwa wakulima wa Tumbaku na kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa kiwanda cha mbolea mkoani Tabora unafanikishwa ili kukabiliana na changamoto hiyo. Nae Meneja wa Bodi ya Tumbaku Kanda ya Tabora, Bw. Albert Charles amesema kuwa licha ya changamoto zilizopo, idadi ya wanunuzi imeongezeka kutoka kampuni tatu msimu wa 2020/2021 hadi kufikia kampuni 18 kwa sasa, hatua inayotoa matumaini kwa wakulima.
Sat, 03 Oct 2026 18:38:00 +0000Page 896 of 1137 · 22740 stories