Search the region
22723 stories
On German Unity Day, Steinmeier laments 'bitter setbacks'
Read the full report from the original source.
RecentlyOn German Unity Day, Steinmeier laments 'bitter setbacks'
Read the full report from the original source.
RecentlyRaila Mausoleum Set for State Handover Ahead of October 7 Dedication
Latest · NATIONAL NEWS
RecentlyGermany news: President laments 'bitter setbacks'
Read the full report from the original source.
RecentlyExperts turn to music to ease pain, stress in palliative care
Read the full report from the original source.
RecentlyLa situation alimentaire devrait rester difficile dans plusieurs régions jusqu’en janvier 2027, selon FEWS NET
Read the full report from the original source.
RecentlyThe Dealmaker: How Simon Mwebaze Built the Ugandan Consortium Taking Over NIC
Read the full report from the original source.
RecentlySalama crash: Families recall final conversations with victims
16 church members were among those who died as relatives gathered for a prayer service in Mikindani
RecentlyMuseveni Insists on Uganda Oil Refinery, Says Crude Exports Alone Are Not Enough
Read the full report from the original source.
RecentlyNRM MPs Seek Museveni’s Financial Support for Legal Fees in 75 Election Petitions
Read the full report from the original source.
RecentlyUhuru joins mourners at the burial of Martha Karua’s father
Leaders gathered in Kirinyaga, to mourn Mwalimu Jackson Karua and stand with his family
RecentlyAFYA YA MAMA KIGAMBONI CITY MARATHON YAHITAJI SH MILIONI 105 KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA
Na MWANDISHI WETU WANANCHI, wadau, taasisi, mashirika, kampuni na watu binafsi wameombwa kujitokeza kuchangia harambee yenye lengo la kukusanya Sh milioni 105 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa muhimu vya afya wilayani Kigamboni, Dar es Salaam. Wito huo umetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Pendo Abdallah Mahalu, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo katika mbio za Afya ya Mama Kigamboni City Marathon, zilizoandaliwa na Taasisi ya Afya ya Mama Foundation kwa lengo la kuchangisha fedha hizo. Mbio hizo zilizoanzia katika Viwanja vya Tungi Madani, karibu na Daraja la Nyerere, wilayani Kigamboni, zilishirikisha wakimbiaji kutoka klabu mbalimbali za marathon nchini, waliokimbia umbali wa kilomita tano na kilomita 21. Pendo amesema fedha hizo zitasaidia kununua vifaa tiba muhimu, vikiwemo mashine za kupima na kufuatilia ishara muhimu za uhai wa watoto, vifaa vya kusaidia upumuaji wa watoto wachanga pamoja na zana za kupima kiwango cha oksijeni katika damu. “Pia zinahitajika seti maalumu za vifaa safi na salama vya kujifungulia kwa ajili ya wajawazito, vitanda vya kujifungulia pamoja na vifaa vya wodi ya uzazi,” amesema Pendo. Amesema Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuwekeza kwa kasi katika sekta ya afya kwa kujenga zahanati, vituo vya afya na hospitali za wilaya kote nchini, ingawa ushiriki wa wadau bado unahitajika. “Ninaipongeza taasisi hii isiyo ya kiserikali ya Afya ya Mama Foundation kwa kuandaa mbio hizi ili kukamilisha pale penye mapungufu na kuhakikisha huduma zinawafikia walengwa,” amesema Pendo. Aidha, amewaomba wadau zaidi kujitokeza kuchangia na kufanikisha harambee hiyo, yenye lengo la kuboresha huduma za afya wilayani Kigamboni. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Afya ya Mama Foundation, Felister Bwana, amesema taasisi hiyo ilianzishwa kwa lengo kuu la kuhakikisha hakuna mama anayepoteza maisha wakati wa kujifungua. “Katika kufuatilia huduma za afya ya uzazi Wilaya ya Kigamboni, taasisi ilibaini kuwa vituo vyetu vya afya na zahanati bado vinakabiliwa na uhaba wa vifaa tiba na miundombinu katika kutoa huduma za msingi kwa mama na watoto wachanga,” amesema Felister. Ameongeza kuwa changamoto hizo ndizo zilizoifanya taasisi hiyo kuandaa mbio hizo zenye kaulimbiu ‘Mama Imara, Taifa Imara’, kwa lengo la kufanya harambee ya kukusanya Sh milioni 105 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba. Mkurugenzi wa Biashara wa Azania Bank, Yahaya Mbanka, amesema benki hiyo imeahidi kuchangia Sh milioni 5 katika kufanikisha mpango huo.
Sat, 03 Oct 2026 10:27:02 +0000TCU YAFUNGUA AWAMU YA TATU YA UDAHILI, PROGRAMU ZENYE NAFASI ZATAFUTWA
Na Janeth Raphael - MichuziTv Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2026/2027, huku waombaji ambao hawakupata nafasi katika awamu zilizopita wakipewa fursa nyingine ya kutuma maombi katika programu ambazo bado zina nafasi. Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa ametoa TAARIFA hiyo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma Leo ambapo amesema, dirisha la kutuma maombi katika awamu hiyo litakuwa wazi kuanzia leo Oktoba 3 hadi Oktoba 9, 2026, baada ya Tume kupokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita pamoja na vyuo ambavyo bado vina nafasi za udahili. Tume imeviagiza vyuo vya elimu ya juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi ili kuwawezesha waombaji kufanya uchaguzi na kutuma maombi kwa wakati. TCU imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kukamilika kwa awamu mbili za awali za udahili, huku ikiwasihi waombaji ambao hawakutuma maombi au hawakupata nafasi katika Awamu ya Pili kutumia fursa hiyo kutuma maombi katika vyuo na programu wanazozipenda. Awamu ya Tatu itafuata ratiba maalum ambapo vyuo vitawasilisha TCU majina ya wanafunzi waliodahiliwa kati ya Oktoba 13 na 14, 2026, kabla ya majina hayo kutangazwa na vyuo husika Oktoba 17, 2026. Aidha, TCU imesema waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili, pamoja na wale ambao hawakuthibitisha udahili wao katika Awamu ya Kwanza, wanatakiwa kuthibitisha udahili katika chuo kimojawapo kuanzia Oktoba 3 hadi 19, 2026. Uthibitisho huo utafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi wa simu au kupitia barua pepe ambayo mwombaji alitumia wakati wa kutuma maombi ya udahili. TCU imeeleza kuwa waombaji ambao hawajapokea namba hiyo wanapaswa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe wenye namba maalum ya siri ili kukamilisha mchakato wa kuthibitisha udahili. Pia, waombaji wameelekezwa kufanya uthibitisho kupitia akaunti walizotumia wakati wa kuomba udahili. Orodha ya waombaji waliodahiliwa katika zaidi ya chuo kimoja inapatikana kupitia tovuti ya TCU. Kwa upande mwingine, TCU imekumbusha kuwa masuala yote yanayohusu udahili au uthibitisho wa udahili yanapaswa kuwasilishwa moja kwa moja kwenye vyuo husika. Vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa za waombaji wanaokumbana na changamoto wakati wa kuthibitisha udahili na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa. Kwa ratiba ya Awamu ya Tatu, maombi ya udahili yatafanyika Oktoba 3 hadi 9, vyuo kuwasilisha majina TCU Oktoba 13 hadi 14, kutangaza majina Oktoba 17, huku uthibitisho wa udahili kwa waliodahiliwa zaidi ya chuo kimoja ukifanyika Oktoba 17 hadi 19, 2026.
Sat, 03 Oct 2026 10:15:26 +0000DKT. MWIGULU AAGIZA UCHUNGUZI MAJENGO YA HOSPITALI YA WILAYA YA BUNDA YALIYOTITIA
▪️︎ Aagiza wahusika kuwajibishwa iwapo uzembe utathibitika ▪️︎ Aelekeza kodi ya klinka iondolewe ili kupunguza bei ya saruji WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kupatiwa taarifa za uchunguzi kuhusu majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Bunda yaliyotitia, akitaka hatua zichukuliwe dhidi ya waliohusika iwapo itathibitika kuwa kulikuwa na uzembe. Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo, Jumamosi, Oktoba 3, 2026, wakati akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Nyamuswa, Wilaya ya Bunda, mkoani Mara, baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Bunda. “Nimeambiwa Waziri wa Afya alishatengeneza timu na ikafanya kazi na TAKUKURU ameshafanyia kazi. Nizipate hizo taarifa ili hawa waliofanya makosa haya wawajibike kule kule walipo. Lazima wawajibike. Hii kuharibu wilaya hii na kuhamishiwa ukaharibu na wilaya nyingine, hii haikubaliki,” amesema. Amesema wakati wa ukaguzi huo amekuta majengo mawili yakiwa yametitia na kupewa maelezo kuwa hali hiyo imesababishwa na uwepo wa maji katika eneo la mradi pamoja na udongo wa mfinyanzi. “Namuuliza kwa nini majengo yametitia? Wanasema kwa sababu yamejengwa karibu na chanzo cha maji. Chanzo cha maji kile kimekuja baada ya kujenga msingi? Si kilikuwepo pale pale? ... Wanasema udongo huu ni wa mfinyanzi,” amesema. Dkt. Mwigulu amesema Serikali itaendelea kufuatilia suala hilo ili kubaini ukweli wa kilichosababisha majengo hayo kutitia na kuhakikisha wananchi hawapati adhabu kutokana na uzembe katika utekelezaji wa miradi ya Serikali. Amesema Serikali pia inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kukamilisha maeneo yaliyobaki ya ujenzi wa hospitali hiyo ili wananchi waendelee kupata huduma za afya katika eneo lao. Katika hatua nyingine, Dkt. Mwigulu amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na kupanda kwa bei ya saruji, ikiwemo kuelekeza kuondolewa kwa kodi kwenye klinka, malighafi inayotumika katika uzalishaji wa saruji. “Nimewaelekeza Mamlaka ya Mapato waondoe kodi kwenye klinka, malighafi inayotumika kwenye uzalishaji wa saruji ili upatikanaji wa saruji uwe wa uhakika na bei iweze kuwa bei himilivu,” amesema. Amesema Serikali inalenga kuhakikisha upatikanaji wa saruji unaendelea kuwa wa uhakika na bei yake inakuwa himilivu kwa wananchi, akibainisha kuwa katika baadhi ya maeneo bei imekuwa ikipanda hadi kufikia zaidi ya Sh. 25,000, Sh. 27,000 na katika baadhi ya mikoa kufikia Sh. 32,000 kwa mfuko. Kuhusu huduma za afya, Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa wananchi hawapaswi kuchangishwa fedha za mafuta kwa ajili ya magari ya Serikali, hususan magari ya wagonjwa yanayotumika kuokoa maisha. “Hatuwezi tukawa na magari ya Serikali yana mafuta, halafu ambulance ya kunusuru maisha ya wagonjwa tuchangishane mafuta. Haya ni mambo ya mazoea ambayo hatutaki kuwa utaratibu wa Serikali,” amesema. Amesema mwananchi yeyote atakayeombwa fedha za mafuta kwa ajili ya gari la wagonjwa anatakiwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua zichukuliwe. Dkt. Mwigulu pia amesisitiza umuhimu wa wagonjwa walio katika hali mbaya kupewa huduma ya dharura mara moja kabla ya kukamilisha taratibu nyingine za kiutawala. “Mgonjwa aliyezidiwa amefika, hatua ya kwanza apelekwe moja kwa moja kwenye kitanda apate huduma. Hata kumwandikisha mtamwandikisha akiwa ameshapata huduma ya kwanza. Kanusuru kwanza maisha yake. Usifanye itifaki kwenye maisha,” amesema. Kuhusu upatikanaji wa dawa, amesema Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, hivyo amewataka viongozi na watendaji wa afya kuhakikisha dawa zinawafikia wananchi waliokusudiwa na matumizi yake yanafuatiliwa ipasavyo. Hospitali ya Wilaya ya Bunda ilianza kutekelezwa tarehe 8 Mei, 2019, ikiwa ni miongoni mwa hospitali 67 za awamu ya kwanza za halmashauri zilizolenga kusogeza huduma za afya za ngazi ya hospitali karibu na wananchi. Hadi sasa, Serikali imetoa jumla ya Sh. bilioni 5.39 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Hospitali hiyo imeanza kutoa huduma mbalimbali, ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje, maabara, afya ya uzazi na mtoto, kujifungua, radiolojia, kulaza wagonjwa, huduma za macho, meno na huduma za dharura.
Sat, 03 Oct 2026 10:16:40 +0000ODPP: No Criminal Charges Were Preferred Against Four Suspects in rape, robbery case
Latest · ACCESS TO JUSTICE
RecentlyTout ce que vous devez savoir sur la Coupe du Monde Féminine de la FIFA 2027
Nous vous présentons, grâce à notre équipe « Ask Me Anything », tout ce qu'il faut savoir sur la Coupe du monde féminine de 2027.
RecentlyGermany: Next president should come from east, says official
Read the full report from the original source.
RecentlyWaziri Mavunde akabidhi gari wa mchimbaji maonyesho ya teknolojia ya madini
Read the full report from the original source.
RecentlyVijana Wabuni Mfumo wa Kidijitali Kudhibiti Taka Dar es Salaam
Read the full report from the original source.
RecentlyRuhuwiko yaendelea kung’ara mitihani ya kidato cha nne na sita
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 903 of 1137 · 22723 stories