Search the region
22655 stories
Eastern Africa Steps Up Regional Fight against Migratory Pests
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto: No residents will be displaced for Lamu refinery
“Lamu refinery, there are no wananchi that we are going to remove from that place. The land that is there is government land,” Ruto said.
RecentlyAéroport de Lomé : ce que l'on sait de l'incident qui suscite de vives réactions sur les réseaux sociaux
Dans sa publication, un journaliste d'investigation révèle que des canalisations des toilettes de l'aéroport international de Lomé ont explosé, éclaboussant des passagers qui attendaient dans le hall d'embarquement.
RecentlyBasic marine course equips officers with water safety and rescue skills
Read the full report from the original source.
RecentlyRwanda, South Sudan take control in TotalEnergies CAF U-23 AFCON qualifiers
Read the full report from the original source.
RecentlyChina-Africa ties Hailed as Uganda Hosts Inaugural African Dragon Boat Racing Competition
Read the full report from the original source.
RecentlyKAMATI YA BUNGE: HATUTAKAA KIMYA MIRADI YA UMWAGILIAJI
MPANDA, KATAVI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imesema haitakaa kimya kuzungumzia mafanikio yanayopatikana katika miradi ya umwagiliaji nchini, ikieleza kuwa imejiridhisha na kazi kubwa inayofanywa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza sekta ya kilimo. Kamati hiyo imesema uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miradi ya umwagiliaji umeanza kuleta mabadiliko kwa wakulima na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao. Akizungumza mkoani Katavi wakati wa ziara ya siku tano ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ambaye pia ni Mbunge wa Njombe Mjini, Mhe. Deodatus Philip Mwanyika, amesema wamejionea kazi kubwa inayofanyika katika Mradi wa Umwagiliaji Mwamkulu. “Ukweli usemwe na hatutakubali kukaa kimya na kufunga midomo. Miradi hii, kwa kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt. Samia, ni lazima ionekane na mahali panapofanya vizuri, maneno ni lazima yawepo,” amesema Mwanyika. Amesema kwa muda mrefu kaulimbiu imekuwa ikisema kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa, lakini Serikali ya Awamu ya Sita imeanza kuifanya kauli hiyo ionekane kwa vitendo kupitia uwekezaji katika miundombinu ya umwagiliaji. “Kilimo kilikuwepo tangu wakati huo na kauli mbiu ilikuwa Kilimo ni Uti wa Mgongo, lakini Rais Samia amekuja kutafsiri na kuonekana kilimo kweli ni uti wa mgongo. Hii miradi ya umwagiliaji inaenda kugusa wakulima na wananchi moja kwa moja na hatutasita kuwasemea pale inapofanya vizuri,” amesema. Mwanyika amesema Mradi wa Umwagiliaji Mwamkulu wenye thamani ya Sh bilioni 33.9 unaotekelezwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda unatarajiwa kubadilisha maisha ya wakulima wa eneo hilo kwa kuwaondolea changamoto walizokabiliana nazo kwa miaka mingi. Kwa mujibu wa Mwanyika, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 83, huku mfereji mkuu wa maji wenye urefu wa kilomita 7.7 ukikamilika kwa asilimia 100. Amesema mifereji mingine mikuu mitatu yenye jumla ya kilomita 14 imekamilika, pamoja na barabara za mashambani zenye urefu wa kilomita 35 na mifereji ya kurudisha maji katika Mto Katuma yenye urefu wa kilomita 18. Aidha, amesema ujenzi wa ghala la kuhifadhi nafaka lenye uwezo wa tani 4,000 umefikia zaidi ya asilimia 90, hatua inayolenga kupunguza upotevu wa mazao baada ya kuvuna. Mwanyika amesema wakati Tanzania ikiweka lengo la kulisha dunia, Katavi ni mkoa wa kimkakati katika uzalishaji wa mazao, hususan mpunga na mahindi, hivyo amewataka wananchi kutumia fursa hiyo na kutunza miundombinu inayojengwa. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amesema mkoa huo ambao zaidi ya asilimia 95 ya wananchi wake wanategemea kilimo, umepokea takriban Sh trilioni 1.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika sekta mbalimbali, huku Sh bilioni 70 zikitengwa kwa ajili ya umwagiliaji. Amesema Mradi wa Mwamkulu ni hatua kubwa katika kukuza kilimo cha umwagiliaji mkoani humo, huku akiomba mabonde mengine nayo yaendelezwe ili kuongeza uzalishaji na tija kwa wakulima. Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuph, amesema mradi huo umeleta matumaini makubwa kwa wananchi na unatarajiwa kuongeza mapato ya Halmashauri. Amesema Wilaya imewashirikisha viongozi wa dini, wazee, vijana wa bodaboda pamoja na vyama vya siasa kutembelea na kujionea uwekezaji huo wa Serikali, huku akiomba kukamilishwa kwa bwawa la kuhifadhi maji ili kuwawezesha wananchi kulima mara mbili kwa mwaka. Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo anayeshughulikia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Eng. Athuman Kilundumya, ameahidi kuwa Tume itaendelea kushirikiana na jamii katika kuhakikisha miradi hiyo inaleta matokeo chanya, huku Wizara ikiendelea kuiwezesha taasisi hiyo kufikia malengo ya Serikali. Kuhusu upatikanaji wa mbegu, Kilundumya ameitaka Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) na Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) kuweka kambi katika eneo la Mradi wa Umwagiliaji Mwamkulu ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wakulima. Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Raymond Mndolwa, amesema mikataba ya Tume hiyo haina gharama za riba, hatua ambayo imeiwezesha Serikali kuokoa zaidi ya Sh bilioni 28 ambazo zingetumika kulipa riba. Mndolwa amesema kutokana na athari za El Niño zinazotarajiwa, Tume imemuelekeza mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anakamilisha kwa wakati na kwa ubora kazi za mashambani kabla ya kukamilisha majengo ya utawala, ili kuwalinda wakulima dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza. Amesema Tume ipo katika mchakato wa kupata mashine zitakazofungwa katika ghala la mpunga lililojengwa katika mradi huo, ili kuwawezesha wananchi kuchakata mazao yao katika eneo hilo. Aidha, ameupongeza uongozi wa mkoa na wilaya kwa ushirikiano wanaoutoa katika kutoa elimu kwa wakulima na kusimamia ukusanyaji wa tozo za ada za umwagiliaji. Kwa niaba ya Mwenyekiti wa skimu na wakulima wa eneo hilo, Mzee Boniphace Chidesela, amesema mradi huo umebadilisha maisha ya wakulima, akieleza kuwa kabla ya mradi walitumia kati ya saa nne na tano kufika mashambani na walilipa Sh10,000 kusafirisha gunia moja la mazao. “Hivi sasa magari yanafika hadi shambani, gharama imeshuka hadi Sh1,000 na safari inachukua dakika 15 tu,” amesema. Uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka wastani wa magunia 20 hadi 35–40 kwa ekari, huku idadi ya wanufaika ikitarajiwa kuongezeka kutoka wakulima 300 hadi 1,500. Akihitimisha ziara hiyo, Mwanyika amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka nguvu kubwa katika sekta ya kilimo, akisema Mradi wa Umwagiliaji Mwamkulu unaonyesha thamani halisi ya fedha za umma ( Value for Money ).
Thu, 01 Oct 2026 17:03:33 +0000Rwanda says telemedicine helped cut maternal deaths by 30% in 2025
Read the full report from the original source.
RecentlyEthiopia: Embassy shut in Eritrea, 10 diplomats expelled
Read the full report from the original source.
RecentlyRAB technician honoured for contribution to bean research
Read the full report from the original source.
RecentlyRais wa zamani wa AfDB ataja vichocheo vitano vya mageuzi ya mashirika ya umma
Read the full report from the original source.
RecentlyWAANDISHI WA HABARI TANZANIA NA OMAN KUIMARISHA TAALUMA YA HABARI,FURSA ZA KIUCHUMI
Na Said Mwishehe, Michuzi TV Tanzania na Oman zimeingia katika hatua mpya ya ushirikiano katika sekta ya habari baada ya kusainiwa kwa Mikataba ya Ushirikiano (MoU) kati ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Oman (OJA), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na Chama cha Wafanyakazi Katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA). Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha taaluma ya uandishi wa habari, kubadilishana uzoefu na maarifa, pamoja na kufungua fursa za kiuchumi na uwekezaji katika sekta ya habari. Mikataba hiyo imesainiwa leo, Oktoba 1, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa Kongamano la Ushirikiano kati ya Wanahabari wa Tanzania na Oman lililowakutanisha waandishi wa habari kutoka nchi hizo mbili. Akizungumza katika kongamano hilo, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Abdallah Kilima, amesema kongamano hilo limefungua ukurasa mpya katika ushirikiano wa Tanzania na Oman, ambao umejengwa katika misingi ya historia, utamaduni, biashara na undugu wa muda mrefu. “Wanahabari wana nafasi muhimu katika kuwajengea vijana uelewa sahihi kuhusu historia ya mahusiano ya nchi hizi mbili. Matukio ya michezo kama Kombe la Ghuba na AFCON yanaweza kutumika katika kubadilishana tamaduni na kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania na Oman,” amesema. Balozi Kilima amesema ushirikiano huo pia utajikita katika mafunzo ya habari za kidijitali, uhakiki wa taarifa na matumizi ya kiwajibikaji ya Akili Unde (AI), akisisitiza umuhimu wa kuwa na mpango kazi wa miezi 12 utakaowezesha kufuatilia utekelezaji wa makubaliano hayo. Kwa upande wake, Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Bin Hilal Bin Saud Al Shidani, amesema uhusiano wa Tanzania na Oman una misingi imara ya kihistoria, huku matumizi ya Kiswahili, Kiarabu na Kiingereza yakirahisisha mawasiliano na ushirikiano kati ya wananchi wa nchi hizo. Amesema zaidi ya waandishi wa habari 50 kutoka Oman wamefika Tanzania kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo, ambalo amesema litasaidia kujenga uwezo, kubadilishana maarifa na kuimarisha maadili ya uandishi wa habari katika kipindi ambacho matumizi ya mitandao ya kijamii yanaendelea kukua. Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Oman (OJA), Dkt. Mohamed bin Mubarak Al Araimi, amesema ushirikiano kati ya Oman na Tanzania una mizizi mirefu ya kitamaduni na kijamii, huku Zanzibar ikiwa sehemu muhimu ya historia ya mahusiano hayo. “Habari haina mipaka na inaweza kuwa daraja linalounganisha watu na mataifa. Hivyo, nawashauri wanahabari kutumia kalamu zao kuhifadhi historia na kusimulia habari za kweli zinazojenga uhusiano kati ya Tanzania na Oman,” amesema. Dkt. Al Araimi amesema kongamano hilo pia limefungua fursa za ushirikiano katika sekta za habari, utalii, uchumi na uwekezaji, akitaja pia mchango wa magazeti ya kihistoria ya Zanzibar, yakiwemo Al-Falaq na Al-Najah . Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema matumizi ya Kiswahili katika kongamano hilo yanaonesha fahari ya lugha hiyo na umuhimu wake katika kujenga uhusiano kati ya jamii za Tanzania na Oman. “TEF ina dhamira ya kuimarisha uweledi, uhuru wa uhariri, uendelevu wa vyombo vya habari na uwajibikaji kwa jamii. Niwahakikishie kwamba magazeti bado yana nafasi katika kutoa habari sahihi licha ya kukua kwa mitandao ya kijamii,” amesema. Aidha, Balile ameunga mkono kuwepo kwa mpango kazi wa miezi 12, huku akipendekeza kuwepo kwa waratibu wawili au watatu watakaosimamia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa. Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Katika Vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA), Musa Juma Siwayombe, amesema kongamano hilo ni hatua mpya kwa kuwa linawashirikisha moja kwa moja wanahabari katika kuendeleza na kuimarisha mahusiano ya Tanzania na Oman. Amesema katika kongamano hilo wamejadili masuala mbalimbali, ikiwemo uhuru wa habari, kubadilishana uzoefu wa kiteknolojia pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya habari. “Niwaombe wawekezaji kutoka Oman kuangalia fursa za kuwekeza katika sekta ya habari nchini Tanzania, ikiwemo televisheni, redio na magazeti,” amesema Siwayombe.
Thu, 01 Oct 2026 16:52:10 +0000Who gets to shape AI? UN debate centres on power, trust and inclusion
Read the full report from the original source.
RecentlyCRDB, Ofisi ya Msajili wa Hazina Zanzibar wasaini makubaliano ya kuimarisha taasisi za umma
Read the full report from the original source.
RecentlyFlydubai co-pilot attack probed
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto: Why Lamu was chosen for Dangote refinery
Ruto said the discussions were influenced by plans to develop a crude oil pipeline from Uganda to the Kenyan coast.
RecentlyCBK seeks power to raid, oust top bosses at payment firms
Read the full report from the original source.
RecentlyGermany news: Merz lauds NATO with Westphalian Peace Prize
Read the full report from the original source.
RecentlyWATCH LIVE: Requiem Mass for Mwalimu Jackson Karua, Martha Karua’s father, at All Saints Cathedral
Read the full report from the original source.
RecentlyVarsity students sensitised on dangers of radicalisation, extremism
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 932 of 1133 · 22655 stories