Search the region
22654 stories
Un premier centre de retour dès l’année prochaine en Afrique
Read the full report from the original source.
RecentlyFinland probes suspected break-ins at politicians' homes
Read the full report from the original source.
RecentlyNairobi among five cities to watch on tech, industry growth
Latest · Africa
Recently8th 100 Most Influential Somalis opens nominations, spotlights Kenya business footprint
economy · 6 hours ago
RecentlyAdvantage Mombasa United as Kariobangi Sharks lose in Playoff
featured · 5 hours ago
RecentlyKenya seeks deeper China trade ties as zero-tariff deal takes effect
News · 4 hours ago
RecentlyBamburi Cement targets cement supply deal for Dangote Lamu refinery
Latest · Business
RecentlyLSK mourns ex-Coast rep Elizabeth Wanjeri
Wanjeri died on Tuesday, September 29, 2026, the society said
RecentlyActivists agree on a multi-sector roadmap to bolster Tanzania’s response to child marriage
DODOMA: STAKEHOLDERS working on child protection and legal reform have agreed on a multi-sector roadmap aimed at strengthening Tanzania’s response…
RecentlyTanzania and Uganda move to make Tanga a new energy hub
Read the full report from the original source.
RecentlyCivil service hiring surpasses exits for the first time in four years
Read the full report from the original source.
RecentlyRuto to Sifuna: "Follow parliamentary procedure to access Dangote refinery deal"
I want to tell you, if you want the agreement, you know how its asked for at Parliament so that its brought, Ruto said.
Thu, 01 Oct 2026 17:49:15 +0300Tanzania, Finland sign MoU that opens a new chapter in mineral research cooperation
DAR ES SALAAM: TANZANIA and Finland have opened a new chapter in mineral research cooperation following the signing of a…
RecentlyUniversity students debate countering violent extremism
Read the full report from the original source.
RecentlyINGINGO Z'INGENZI Z'IMPAMVU YO GUSABA GUHINDUZA AMAZINA
Thu, 01 Oct 2026 17:10:40 +0200Tanzania, Algeria translate presidential directives into practical cooperation across five strategic areas
ALGERIA: For years, Tanzania and Algeria have described their relationship in the language of friendship, solidarity and strategic partnership. Now,…
RecentlyJKCI invites Tanzanian athletes to undergo free health screenings and free treatment
Read the full report from the original source.
RecentlyDKT. MWIGULU: TANZANIA NA QATAR BADO TUNA FURSA NYINGI ZA KIUCHUMI
-Apigia chapuo utekelezaji wa DIRA 2050 WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema bado kuna fursa nyingi za ushirikiano wa kiuchumi baina ya Taifa la Qatar na Tanzania ambazo zikitumiwa vizuri zitawanufaisha raia wa nchi zote mbili. “Bado tuna fursa nyingi ambazo tunaweza tukanufaika nazo kama tutatekeleza baadhi ya shughuli za kiuzalishaji. Tanzania kama lango la Afrika Mashariki, Kusini na Kati na Qatar kama lango la Mashariki ya Kati na Umoja wa Nchi za Ghuba tulikubaliana kuwa tukichangamkia fursa zote zinazojitokeza, tutaongeza ushiriki wa wananchi wa nchi zote mbili,” alisema. Alikuwa akizungumza na Rais na Mtendaji Mkuu wa Power International Holding (PIH), Bw. Ramez Al-Khayyat na baadhi ya viongozi wakuu wa taasisi hiyo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Lusail, jijini Doha. Waziri Mkuu alimshukuru Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH kwa kuonesha nia ya dhati ya kuwekeza katika sekta ambazo DIRA 2050 imeyaainisha kama maeneo ya kipaumbele. “Tunashukuru kwamba hii kampuni imeonesha nia ya kuwekeza kwenye maeneo yaliyotajwa katika DIRA 2050 ambayo na sisi tumeyawekea kipaumbele. Wameonesha nia ya kushiriki DIRA yetu kupitia utekelezaji wa fursa zilizopo. Tumekubaliana kwamba mawaziri waliopo wakiongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Kapinga wafuatilie kwa karibu ili utekelezaji uanze mara moja.” Kwa upande wake, Rais na Mtendaji Mkuu wa PIH, Bw. Ramez Al-Khayyat alimweleza Waziri Mkuu kwamba Power International Holding ni kampuni kubwa ya kimataifa inayomilikiwa na watu binafsi ambayo inaendesha kampuni tanzu 400 zenye wafanyakazi 65,000 katika nchi 26. Kati ya nchi 26, za Afrika ni Misri, Libya, Morocco, Algeria, Mauritania na Rwanda. Alisema wameshaingia makubaliano na Ethiopia (ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa) na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 400). “Utendaji kazi wa taasisi yetu umegawanyika katika makundi makubwa saba ya kibiashara yanayoendeshwa kimataifa na yenye kampuni tanzu 400 na wafanyakazi 65,000. Kwa sehemu kubwa, shughuli zetu zinajihusisha na madini, ujenzi wa miundombinu mikubwa, ujenzi wa majengo ya makazi pamoja na hoteli, kilimo na viwanda, utalii na utoaji huduma za mawasiliano,” alisema Mapema, akitoa taarifa kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Mkurugenzi Mkuu wa TANTRADE, Bw. Ephraim Mafuru alisema kwa muda mrefu Tanzania ilikuwa ikisafirisha nyama ya mbuzi na kondoo kwenda nchi za Ghuba lakini kwa sasa inaweza kufanya vizuri zaidi endapo itaongeza mazao ya kilimo na madini hasa ya dhahabu. “Tunalo soko kubwa la dhahabu ambalo kimsingi halijatumiwa. Tunajua soko liko hapa katika Ghuba. Lakini pia kuna fursa kubwa kwenye mchele ambao unaweza kutuingizia dola bilioni 3.9. Mwaka jana, tulizalisha tani milioni 3.4 za mchele na tukatumia tani milioni 1.8 tu. Maana yake ni kwamba tuna zaidi ya tani milioni 1.6 ambazo tunaweza kuzisambaza kwa watu milioni 3.4 waishio nchini Qatar.” Akielezea kuhusu fursa za uwekezaji nchini Tanzania, Bw. Mafuru aliyataja maeneo hayo kuwa ni nishati, LNG, utalii, mbogamboga na matunda, maua, uzalishaji wa malisho ya mifugo pamoja na mazao yanayotokana na uchumi wa bluu. Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu alifuatana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ngwaru Maghembe, Katibu Wakuu (OR-Uwekezaji), Wakuu wa Mikoa ya Pwani na Dodoma, Wabunge Esther Matiko na Subira Mgallu na watendaji wengine wa Serikali.
Thu, 01 Oct 2026 14:44:38 +0000RAIS DKT SAMIA AAPISHA VIONGOZI,AONGOZA BARAZA LA MAWAZIRI
Thu, 01 Oct 2026 15:02:24 +0000KAMATI TENDAJI NA ELEKEZI ZA MAAFA TANGA ZAJIPANGA KUKABILIANA NA EL NINO
Na; Mwandishi – Wetu Tanga Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Ndugu Rashid K. Mchatta amesema Mkoa wa Tanga umejipanga kikamilifu kupitia Kamati zake za Wataalamu na Kamati Elekezi za Usimamizi wa Maafa za Mkoa katika kukabiliana na Mvua za El Nino zinazotabiriwa kuanza kunyesha mapema mwezi huu. Bw. Mchatta ameyasema hayo mapema leo Mkoani Tanga Alipokutana na Timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na wenye Ulemavu inayoongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Sehemu ya Afya Moja Dkt. Salum Manyata, pamoja na kamati tajwa Mkoani hapo Tarehe 1 Oktoba 2026. Bw. Mchatta alibainisha kuwa tahadhari ya Mvua za El Nino na utabiri wa hali ya hewa umetoka mapema sana jambo ambalo limeweza kutoa nafasi kwa Mkoa kutoa tahadhari ya mapema kwa wananchi na Taasisi husika na kuchukua hatua stahiki kwa wakati ikiwemo hatua za haraka za kukabiliana na jambo hilo sambamba na upatikanaji wa rasilimani wezeshi. Aliendelea kusema kuwa katika kujiandaa kukabiliana na janga hilo katika Mkoa wa Tanga kuna Taasisi ambazo zinaonekana kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na Wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA, Wakala wa Barabara Nchini TANROADS na Shirika la Reli Nchini TRC . “Kwa upande wa Usafi wa Mazingira, Mkoa umeshatoa Miongozo na maelekezo kuhusiana na usafi na Usimamizi wa Mazingira pamoja na kuchukua tahadhari ya suala zima la El Nino.”Alisisitiza Bw. Mchatta Imeelezwa kuwa Mkoa wa Tanga umetambua maeneo hatarishi yanayoweza kuathiriwa na mvua na kuanza kufanyiwa kazi kabla ya kuanza kwa mvua zinazotarajiwa kunyesha. Kikao kazi hiki Mkoani Tanga kitaambatana na ziara ya kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa kwa Mkoa kuhusu kujiandaa na kukabiliana na madhara ya El Nino kwa mwaka, 2026.
Thu, 01 Oct 2026 15:04:06 +0000Page 934 of 1133 · 22654 stories