Search the region
22652 stories
Il est trop tôt pour dire si l'Iran est impliqué dans l'attaque du vol Dubaï-Tel Aviv, a déclaré le Premier ministre israélien
Un pilote qui a poignardé un autre pilote à bord d'un avion à destination d'Israël fait l'objet d'une enquête en Arabie saoudite, a déclaré Benjamin Netanyahu.
RecentlyTuchel: Hatutampata Kane mwingine
KOCHA wa England, Thomas Tuchel amesema haitakuwa rahisi kwa timu hiyo kumpata mshambuliaji mwingine wa kiwango cha nahodha wake, Harry Kane ambaye anaendelea kuvunja rekodi na kuweka historia...
RecentlyMambo matano Ngao ya Jamii Wanawake 2026
Read the full report from the original source.
RecentlyVietnam yajenga uwanja mkubwa wa kushangaza
UWANJA mkubwa zaidi wa soka duniani unaendelea kujengwa kwa kasi mjini Hanoi, Vietnam, huku picha mpya zikionyesha namna eneo hilo linavyoanza kubadilika na kuwa moja ya viwanja vya kuvutia zaidi...
RecentlyMsuva asiwaze kwanza kuvunja rekodi
Read the full report from the original source.
RecentlyKiemba, Domayo zamu yenu kuchambuliwa
Read the full report from the original source.
RecentlyGirumugisha Jean-Claude : et si Msauza s’appelait Vinicius
Il y a des jours où le football cesse d'être un sport. Il devient une déclaration. Imaginez la scène si, mardi 29 septembre 2026, au Stade Intwari, ce but avait été signé Vinicius Junior. Les chaînes du monde tourneraient en boucle. On parlerait de génie pur. Mais il ne s'appelait pas Vinicius. Il s'appelle Jean-Claude Girumugisha . On le surnomme Msauza . Il est Burundais.
Thu, 01 Oct 2026 14:52:31 +0000Renee Good's family sues Trump admin over fatal ICE shooting
Read the full report from the original source.
RecentlyArusha sets stage for landmark IPU Assembly
Read the full report from the original source.
RecentlyCEO’s WARUDI NYUMBANI NGORONGORO.
Na mwandishi wetu, Ngorongoro Watendaji Wakuu wa Taasisi za Serikali na mashirika ya Umma wametembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kufanya utalii wa ndani kuona vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo Ngorongoro ambayo ni kivutio bora cha utalii Africa mwaka 2023 na 2025. Akizungumza wakati wa ziara hiyo kaimu mwenyekiti wa CEOs Forum ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) Bw. Ephraim Balozi Mafuru amesema pamoja na utalii ziara hiyo imewapa nafasi ya kutumia jukwaa la wakuu wa taasisi kujadili na kuatafakari kwa pamoja namna bora ya kutekeleza dira ya taifa ya maendeleo 2050. “Kama viongozi tumeona tuje kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutembelea Ngorongoro ili kuongeza hamasa kwa jamii katika kuchangia kukuza sekta ya utalii, tumepata fursa ya kujadili michango ya taasisi za serikali na binafsi katika kufanikisha Dira ya 2050”. alisema Mafuru Ziara hiyo imefanyika mara baada ya kukamilika kwa Kikao Kazi cha CEO Forum 2026, kilichofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), na kuwakutanisha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ufanisi wa utendaji, uwajibikaji na mchango wa taasisi za umma katika kufanikisha utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Meneja uhusiano wa NCAA Hamis Dambaya ameeleza kuwa ujio wa viongozi hao umekuwa ni fursa muhimu ya kuendelea kuitangaza Ngorongoro kama eneo lenye thamani kubwa ya uhifadhi, utalii, historia na elimu huku ikiendelea kuimarisha uelewa wa wadau kuhusu kuendeleza utalii endelevu na kuhakikisha rasilimali zinazopatikana ndani ya eneo la Ngorongoro zinaendelea kutoa manufaa kwa Taifa bila kuathiri thamani yake kwa vizazi vijavyo.
Thu, 01 Oct 2026 14:48:28 +0000RC MAKALLA: ARUSHA IPO TAYARI KUWA MWENYEJI WA BUNGE LA DUNIA
•Asema maandalizi yamekamilika, washiriki zaidi ya 2,000 kuhudhuria kutoka mabunge 183 Na Vero Ignatus, Michuzi TV – Arusha Mkuu wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Gabriel Makalla, amemhakikishia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Balozi Anda Cristina Filip, kuwa Mkoa wa Arusha umekamilisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani, unaotarajiwa kuanza Oktoba 5, 2026, katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). Akizungumza leo, Alhamisi, Oktoba 1, 2026, alipokutana na Balozi Anda ofisini kwake jijini Arusha, RC Makalla amesema mkoa umejiandaa kwa muda mrefu kuhakikisha mkutano huo unafanyika kwa mafanikio ambapo Mkutano huo ni wa kihistoria kwa Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza kuandaa mkutano huo wa kimataifa. RC Makalla amesema kuwa usalama wa washiriki ni kipaumbele, akisisitiza taasisi mbalimbali zimeunganisha nguvu kuhakikisha maandalizi yote muhimu yanakamilika kwa wakati ambapo mkutano huo unatarajiwa kutoa fursa kwa wajumbe kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya kibunge na kuimarisha ushirikiano kati ya mabunge ya nchi wanachama. Balozi Anda pia ameeleza matumaini yake kuwa mkutano huo utafanikiwa na washiriki watapata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini, hatua inayoweza kuwapa fursa ya kuifahamu Tanzania na vivutio vyake. Kufanyika kwa mkutano huo jijini Arusha kunaipa Tanzania fursa ya kuandaa jukwaa muhimu la kidiplomasia na kibunge linalowakutanisha viongozi kutoka mataifa mbalimbali. Kwa Arusha, maandalizi hayo yanaweka mkoa katika nafasi ya kupokea wageni wa kimataifa, huku mafanikio ya mkutano yakitarajiwa kutegemea ushirikiano wa taasisi husika, usalama na utekelezaji wa ratiba ya shughuli zilizopangwa.
Thu, 01 Oct 2026 14:42:59 +0000DKT. TULIA: MKUTANO IPU FURSA TANZANIA KUJITANGAZA DUNIANI
Na Seif Mangwangi, Michuzi Tv Arusha Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, amesema mkutano wa Umoja huo unaofanyika jijini Arusha ni fursa kubwa kwa Tanzania kujitangaza kimataifa kupitia diplomasia ya kibunge, utalii na namna nchi inavyoshirikisha makundi mbalimbali katika uongozi na meza za maamuzi. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo 1Oktoba 2026, Jijini Arusha alipotua kwaajili ya maandalizi ya mkutano huo unaoanza Oktoba 5 mwaka huu, Dkt. Tulia amesema mkutano huo unaowakutanisha wabunge na viongozi kutoka zaidi ya nchi 180 duniani. Dkt Tulia amesema mkutano huo umeifanya Tanzania kuwa sehemu muhimu ya mijadala ya kimataifa, huku wajumbe hao wakipata nafasi ya kujifunza kuhusu Tanzania na Watanzania nao kupata fursa ya kujifunza kutoka kwa mataifa mbalimbali. Amesema uwepo wa zaidi ya wageni 2,000 nchini ni fursa ambayo Tanzania inapaswa kuitumia kuwaonyesha wageni hao uwezo wa nchi katika kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, pamoja na ukarimu wa Watanzania. Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, mkutano huo pia umeipa Tanzania nafasi ya kuonyesha namna inavyoshirikisha wanawake katika uongozi, akibainisha kuwa nchi inaongozwa na mwanamke, jambo ambalo ni sehemu ya uzoefu ambao dunia inaweza kujifunza kutoka Tanzania. Amesema pamoja na wanawake, Tanzania imekuwa ikitoa nafasi kwa vijana na watu wenye ulemavu kushiriki katika michakato ya maamuzi, akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha makundi mbalimbali yanapata nafasi katika uongozi. Dkt. Tulia amesema Tanzania inapaswa kutumia uwepo wa wajumbe hao kuhakikisha wanarejea tena nchini baada ya mkutano, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa shughuli za utalii, biashara na maeneo mengine ya uwekezaji. Amesema kuchaguliwa kwa Arusha kuwa mwenyeji wa mkutano huo kumeipa Tanzania nafasi ya kuwawezesha wageni kuona kwa macho yao vivutio vya utalii ambavyo awali walikuwa wakivisikia kupitia simulizi. “Tunataka warejee tena, si kwa ajili ya mikutano pekee, bali pia kwa ajili ya utalii na shughuli nyingine,” amesema Dkt. Tulia. Ameeleza kuwa mkutano huo pia ni sehemu ya kuimarisha diplomasia ya kibunge ya Tanzania, huku wajumbe kutoka mataifa mbalimbali wakipata nafasi ya kufahamu namna Tanzania inavyoendesha shughuli zake za kibunge na kushughulikia masuala ya kitaifa na kimataifa. Katika hatua nyingine, Dkt. Tulia amesema Tanzania imechangia mabadiliko mbalimbali ya kanuni na taratibu za uendeshaji wa Umoja wa Mabunge Duniani katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wake. Amesema mabadiliko hayo yamewezesha Umoja huo kupata nafasi pana zaidi ya kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo wakati mwingine wajumbe walilazimika kuchagua suala moja pekee kati ya masuala kadhaa yaliyokuwa yakihitaji kujadiliwa. Dkt. Tulia ametolea mfano majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali duniani, akisema mfumo ulioboreshwa sasa unaruhusu mijadala kuhusu changamoto hizo kufanyika kwa upana bila kulazimika kuacha suala moja ili kujadili jingine. Amesema mabadiliko hayo pia yameongeza nafasi ya kujadili masuala ya amani na usalama yanayoendelea katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Sudan, Ukraine, Iran na maeneo mengine. Kwa mujibu wa Dkt. Tulia, Tanzania inaona umuhimu wa mijadala hiyo kwa kuwa migogoro na changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo zinaweza kuwa na athari kwa nchi nyingine na jamii ya kimataifa kwa ujumla. Aidha, amesema Tanzania imechangia katika kukuza ushiriki wa wanawake ndani ya mabunge duniani, akieleza kuwa baadhi ya nchi ambazo awali hazikuwa na wanawake katika mabunge yao zimeanza kufanya mabadiliko baada ya juhudi za kuhamasisha ushiriki wao. Dkt. Tulia amesema katika mkutano huo, ambao unatarajiwa kuwa na zaidi ya wageni 2,000, umewekwa utaratibu wa kuhakikisha wanawake na vijana wanashiriki, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhakikisha mijadala ya Umoja wa Mabunge Duniani inawakilisha makundi mbalimbali ya jamii.
Thu, 01 Oct 2026 14:43:40 +0000Stanbic, SBG Securities Launch Pension Fund Management Service
Read the full report from the original source.
RecentlySafaricom taps Pesapal’s 30,000 POS terminals to take M-PESA contactless
Read the full report from the original source.
RecentlyWATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA UFANISI
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026. Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele na Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima. Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar akihutubia wakati wa ufungaji wa mafunzo Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 kwa watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi 01 Oktoba, 2026. Katikati ni Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele. Mkurugenzi wa Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima. Mwenyekiti wa Mafunzo, Ndg Godfrey Mnyamale akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. *****Na. Mwandishi Wetu, Tabora Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa uchaguzi kuhakikisha wanafanya kazi kwa ufanisi, weledi na kujitoa ili kufanikisha zoezi la uchaguzi kwenye Jimbo la Chamwino na kata 11 za Tanzania Bara. Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohammed Abubakar Mkoani Tabora leo tarehe 01 Oktoba, 2026 wakati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 29 Septemba hadi o1 Oktoba, 2026. “Ni matazamio ya Tume kwamba, baada ya kupatiwa mafunzo haya, mtatekeleza majukumu yenu kwa ufanisi na weledi mkizingatia ratiba ya utekelezaji ili kufanikisha uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Chamwino na Madiwani katika kata 11 za Tanzania Bara, unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba, 2026,” amesema. Dkt. Zakia amewakumbusha watendaji hao kuwa shughuli zote za uchaguzi zinaongozwa na Katiba, sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi na maelekezo ya Tume na kuwasihi kuendelea kutenga sehemu ya muda wao kusoma Katiba, sheria na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na Tume ili yawaongoze katika kusimamia uchaguzi utakaokuwa huru na wa haki. Amesisitiza kuwa ili ufanisi uwepo ni muhimu watendaji hao wakazingatia sifa na uwezo wakati wa kuteua na kuajiri watendaji wa vituo vya kupigia kura kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni. “Kuhusu utaratibu wa kupata watendaji wa vituo, tunayo imani kuwa mtateua na kuajiri watendaji wenye sifa na uwezo wa kufanya kazi hii muhimu kwa mustakbali wa Taifa letu. Jambo hili limekuwa likisisitizwa tokea siku ya kwanza ya mafunzo kwa kuwa hao ndio watakaosimamia zoezi la kupiga kura na kuhesabu kura vituoni. Kazi ambayo inahitaji umahiri, umakini na weledi katika kuitekeleza,” amesema Dkt. Zakia. Amewataka watendaji hao kuhakikisha kuwa mafunzo ya watendaji wa vituo yanafanyika kwa ufanisi na weledi katika tarehe zilizopangwa kwenye ratiba ya utekelezaji wa shughuli za uchaguzi. Mafunzo hayo yamewahusisha Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi Ngazi ya Jimbo, Wasimamizi wa Uchaguzi Ngazi ya Kata, Maafisa Uchaguzi, Maafisa Ununuzi na Wahasibu. Kata 11 za Tanzania Bara zitakazofanya uchaguzi wa Udiwani ni Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya; Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro. Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe. Mkufunzi akiwasilisha mada kuhusu mapokezi na utunzaji wa vifaa vya Uchaguzi. Mmoja wa wakufunzi akiwasilisha mada kuhusu matumizi ya fedha za Uchaguzi. Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini. Mkufunzi wa mafunzo hayo akiwasilisha mada kuhusu usimamizi wa fedha za Uchuzi. Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini. Washiriki mbalimbali wa mafunzo hayo wakifatilia mafunzo kwa umakini.
Thu, 01 Oct 2026 14:36:25 +0000As Roko Construction Falters, is Homegrown SMS Rising to Become Uganda’s Leading Contractor?
Read the full report from the original source.
RecentlyRaila month: Team warns against illicit fundraisers
It is alleged that some people were already taking advantage of the anniversary period to solicit funds.
RecentlyMechi za Kimataifa Zaja Kivingine Kabisa
VIWANJA mbalimbali kuwaka moto siku ya leo kushuhudia mitanange ya moto kwelikweli. Pointi 3 zinawaniwa na timu tofauti tofauti. Unasubiri nini kutengeneza jamvi lako la ushindi? Mechi za Kimataifa zinaendelea ambapo kule Ulaya michuano ya UEFA Nations League inaendelea ambapo Ujerumani atakuwa nyumbani kumenyana vikali dhidi ya Serbia ambapo kwenye kundi lao wao ndio wapo nafasi ya mwisho huku tofauti yao ikiwa ni pointi 1. Timu hiyo ya Ujerumani chini ya Klopp inaingia kwenye mchezo huu ikiwa katika kipindi cha mpito. Jürgen Klopp amechukua timu hiyo baada ya Kombe la Dunia la 2026 na anajaribu kujenga timu yenye nguvu zaidi kuelekea Euro 2028. Katika michezo yake ya mwanzo, Klopp amekuwa akitafuta namna bora ya kuchanganya wachezaji wenye uzoefu na vipaji vipya. Suka jamvi mechi hii. Kwa upande wa Serbia ni timu yenye nguvu kimwili na inaweza kuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushtukiza. Wanahitaji kuwa na nidhamu katika ulinzi na kutumia vizuri mipira ya mwisho wanapopata nafasi. Kiungo kitakuwa eneo muhimu kwa sababu timu itakayolitawala eneo hilo inaweza kupata udhibiti mkubwa wa mchezo. Kila timu inahitaji kupata ushindi siku ya leo, kwani pointi 3 ni muhimu sana kwa pande zote mbili. Je nani kushinda?. Jisajili hapa. Mkwanja mnono upo kupitia michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits , Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Mtanange mwingine ni huu wa Ugiriki dhidi ya Uholanzi ambapo hawa wote wapo kwenye Kundi A na kila timu leo hii inahitaji kupata ushindi kwenye mchezo huu ili iweze kujiweka kwenye nafasi nzuri kundini. Ugiriki ni timu ambayo inaweza kuingia mchezoni kinidhamu zaidi, na kufanya mashambulizi ya kushtukiza pale inapopata nafasi. Ufanisi wao mbele ya lango utakuwa muhimu, kwa sababu huenda wasipate nafasi nyingi za kufunga kutokana na mpinzani ambaye wanaenda kukutana naye. Kwa upande wa Uholanzi wao chini ya kocha mkuu Xavi Hernandezi, nguvu yao kubwa iko kwenye kasi ya kushambulia, ubunifu wa viungo na uwezo wa kutumia nafasi kwenye maeneo ya pembeni. Wanatarajiwa kujaribu kuutawala mchezo mapema na kuilazimisha Ugiriki kujilinda kwa muda mrefu. Hata hivyo, wakishindwa kutumia nafasi zao, Ugiriki inaweza kuwaadhibu kupitia counter-attacks. Hivyo, mchezo huu unaweza kuamuliwa zaidi na umakini wa ulinzi na ubora wa kumalizia nafasi. Tofauti yao mpaka sasa ni 2 pekee huku takwimu zikionesha kuwa mechi mbili mara ya mwisho kukutana Uholanzi ameondoka na ushindi meci zote mbili, hivyo huenda hii ndio mechi ya kisasi kwa Ugiriki. Beti hapa. Lakini pia mechi nyingine ambao unaweza kukupatia pesa ni Denmark dhidi ya Ureno ya Cristiano Ronaldo ambao kwenye mechi mbili wameshinda zote hivyo wameanza vyema kabisa kwenye michuano hii. Denmark inaingia kwenye mchezo huu ikiwa na faida ya kucheza nyumbani, hivyo itahitaji kutumia nguvu na kasi ya wachezaji wake wa pembeni kuiwekea Ureno presha kwani wana wachezaji wengi wazuri wakiwemo Højlund na wengine. Ureno ina ubora mkubwa katika eneo la kiungo kupitia Bruno Fernandes, Vitinha na Joao Felix, pamoja na uzoefu wa Cristiano Ronaldo katika safu ya ushambuliaji hivyo inawafanya kuwapa faidi zaidi. Hata hivyo, kucheza ugenini dhidi ya Denmark kutahitaji umakini mkubwa katika ulinzi na matumizi mazuri ya nafasi. Kwa ujumla, tunatarajia mchezo wenye ushindani mkubwa ambao unaweza kuamuliwa na ubora wa timu katika dakika za mwisho. Nani kushinda leo?. Jisajili hapa.
Thu, 01 Oct 2026 07:00:00 +0000Jungle Temple Yafungua Milango Ya Hazina Meridianbet
KUNA wakati safari haianzi kwa kufunga mizigo, bali kwa kubofya mchezo na kuingia kwenye dunia nyingine kabisa. Wapenzi wa kasino mtandaoni ya Meridianbet sasa wana safari mpya ya kuifuata kupitia Jungle Temple, mchezo wa Expanse unaopatikana Meridianbet . Safari hii inakufikisha ndani ya msitu wa kale uliojaa mahekalu yaliyofichika, siri za ajabu na hazina inayosubiri kugunduliwa. Kila mzunguko unafungua ukurasa mwingine wa safari, huku msisimko ukiongezeka kadri mchezo unavyoendelea. Jungle Temple si mchezo wa kawaida unaokuacha ukitazama skrini bila hamu ya kujua kitakachofuata. Umeundwa kwa mchanganyiko wa historia, fumbo na teknolojia ya kisasa, ukimuweka mchezaji katikati ya safari ya kutafuta hazina. Kila upande wa mchezo umejaa mandhari ya msitu wa kale, huku alama na vitu mbalimbali vikifanya kila mzunguko kuwa na simulizi lake. Ndani ya Meridianbet Kasino , sasa kuna sehemu mpya ya kupeleka burudani yako kwenye kiwango kingine. Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi. Kadri safari inavyosonga, ndivyo siri zaidi zinavyofunguka. Jungle Temple imejaa vipengele vya bonasi vinavyoweza kuongeza msisimko na kufanya kila raundi ionekane kama hatua muhimu kuelekea hazina iliyofichwa. Hapo ndipo mvuto wa mchezo unapoongezeka, kwa sababu hujui ni mzunguko upi utakaokuja na tukio la kusisimua. Ni safari inayokualika kuendelea kuchunguza huku ukifurahia kila hatua ndani ya dunia hii ya ajabu. Kwa Meridianbet, kuleta michezo mipya na yenye ubora kwa wapenzi wa kasino ni sehemu ya safari yake ya kuendelea kuboresha burudani. Jungle Temple imewasili ikiwa na ladha tofauti, ikiwaunganisha mashabiki wa sloti na mazingira ya msitu wa kale yaliyojaa siri na matarajio. Kama unapenda michezo yenye mandhari ya kipekee, changamoto na hisia ya kugundua kitu kipya kila unapocheza, basi mlango wa Jungle Temple umefunguliwa kwa ajili yako. Sasa ni wakati wa kuingia msituni na kuanza safari yako kupitia Meridianbet . Jungle Temple inakusubiri ikiwa na mahekalu yaliyofichika, siri za kale na nafasi za kugundua vipengele mbalimbali vya mchezo. Fungua mchezo leo na uone kinachokusubiri nyuma ya mlango wa hekalu.
Thu, 01 Oct 2026 05:00:00 +0000Askari watatu wajeruhiwa gari la polisi likipinduka Kilimanjaro
Read the full report from the original source.
RecentlyPage 935 of 1133 · 22652 stories