Unganishwa

Search the region

22611 stories

Uncategorized · DW Rwanda

Germany news: Cabinet approves care reform bill

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · PML Daily

Equal Earth designers to help bring ‘true size’ Africa map to schools

The three cartographers who designed the Equal Earth world map have agreed to help African governments put a new UN resolution into practice. The resolution calls for maps that show Africa...

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

Airtel Uganda Pays UGX42.6bn Dividend to NSSF, Boosting Value for Savers

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · CEO East Africa

President Ruto, Billionaire Dangote Launch $16 Billion East Africa Refinery Project in Kenya

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

La pluie et le vent détruisent 11 maisons dans le district de Ngoma

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Uganda Showcases Its Offerings at Oromia Tourism Week 2026 in Addis Ababa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · SoftPower News

Uganda’s Refinery Will Be Built, Tanzania Cooperation on Tanga Stands, Maintains Museveni at Dangote Lamu Groundbreaking

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Tob Cohen's murder trial: Bartenders recount his final moments before disappearance

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

What happened on board the rerouted flydubai plane?

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

MP Ng’ang’a: Keep politics out of Dangote refinery

Ng'ang'a said the project should be viewed from the perspective of its impact on ordinary Kenyans

Recently
National · Issa Michuzi

SERIKALI KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI USHIRIKI WA WADAU KATIKA MAENDELEO YA MAKAZI NCHINI

Na Munir Shemweta Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ushiriki wa wadau katika maendeleo ya makazi, kwa kuzingatia sera, sheria na mipango ya kitaifa. Hayo yameelezwa leo tarehe 30 Sept 2026 na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo wakati wa sherehe za miaka 40 ya UN Habitat for Humanity Tanzania jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yameambatana pia na kampeni ya ‘’Opening the door campaign’’ pamoja na uzinduzi wa mpango mkakati wa miaka mitano ya shirika hilo (Strategic Plan 2025-2029). Mhe. Dkt Leonard Akwilapo amesema, Serikali, inatamani kuona Tanzania ambayo kila familia inapata fursa ya kuishi katika makazi salama, bora, yenye huduma muhimu na yanayomudu uwezo wa kiuchumi. Amebainisha kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha kuwa watanzania wanakuwa na makazi salama. Amesema, wizara yake inafanya juhudi pia za Kuimarisha upangaji na usimamizi wa ardhi; Urasimishaji wa makazi yasiyopangwa na Kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi na wadau wengine kushiriki katika utoaji wa makazi bora na nafuu nchini. Amelipongeza Shirika la Habitat for Humanity Tanzania kwa kuandaa na kuzindua Mkakati wake wa Miaka Mitano (Strategic Plan 2025-2029) mkakati alioueleza kuwa, utatoa fursa ya kuangalia miaka ijayo kwa mtazamo mpana zaidi. Akielezea kampeni ya “ Opening the Door Campaign” ya Habitat for Humanity amesema, kampeni hiyo inao ujumbe mzito na muhimu ambapo ametoa rai kuwa kampeni hiyo itumike kuhamasisha wadau wengi zaidi kuwekeza katika makazi na fursa zinazotokana na makazi bora. ‘’Ninaamini kwamba mafanikio ya kampeni hii yatategemea uwezo wetu wa kuunganisha nguvu za wadau mbalimbali na kuzifanya rasilimali zifike kwa wananchi wenye uhitaji zaidi ili lengo la kuwafikia watu millioni tatu na laki mbili ifikiwe’’. Amesema Ametoa wito kwa sekta binafsi, taasisi za fedha, wafadhili, mashirika ya kimataifa, wataalamu na wananchi kuendelea kushirikiana na Habitat for Humanity Tanzania katika kufikia malengo yao haya. Amesema, Wizara yake inapongeza kuanzishwa kwa Mkakati wa Miaka Mitano na “Opening the Door Campaign” ambapo ameeleza kuwa, iwapo utatekelezwa vyema utachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto ya makazi nchini. Mkurugenzi wa Taifa wa Un Habitat for Humanity Tanzania Bi. Magdalena George amesema shirika hilo limekuwa msaada mkubwa kwa jamii hususan katika upande wa makazi bora na kubainisha kuwa tayari shirika hilo limewafikia zaidi ya watu milioni 1.3. Hata hivyo, amesema Pamoja na shirika hilo kutilia mkazo ujenzi wa nyumba salama na za gharama nafuu pia linaangalia vifaa vya ujenzi ili jamii iweze kumudu gharama za ujenzi. Kwa upande wake Mlezi wa Un Habitat for Humanity Tanzania ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa amesema, amekuwa akilishawishi Shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania kujenga nyumba za wahitaji wasiojiweza na kutolea mfano wa ujenzi wa nyumba eneo la Chamwino Mkoani Dodoma na kueleza kuwa ujenzi huo uliacha alama. Shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania mbali na kushiriki kusaidia ujenzi wa nyumba kwa wasiojiweza na wenye uhitaji pia linashiriki kwenye miradi ya majisafi na usafi wa mazingira pamoja na Matumizi ya Nishati Safi ya Jua katika mashule. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akipata maelezo ya utekelezaji miradi mbalimbali ya shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi wa Taifa wa shirika hilo Bi. Magdalena George wakati wa sherehe za miaka 40 zilizofanyika jijini Dar es Salaam Sept 30, 2026. Kushoto ni mlezi wa shirika hilo Mama Anna Mkapa. aziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizindua kampeni ya “Opening the Door Campaign” wakati wa sherehe za miaka 40 ya shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam Sept 30, 2026. Kushoto ni mlezi wa shirika hilo Mama Anna Mkapa na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Bi. Neema Ndikumwani. Mmoja wa wanufaika na miradi ya Shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania akielezea namna alivyonufaika na miradi ya shirika hilo wakati wa sherehe za miaka 40 ya Un Habitat for Humanity Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akizungumza katika sherehe za miaka 40 ya shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam Sept 30, 2026. Kushoto ni mlezi wa shirika hilo Mama Anna Mkapa. Mlezi wa shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania ambaye ni mke wa Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu Mama Anna Mkapa akizungumza wakati wa sherehe za miaka 40 ya shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania zilizofanyika jijini Dar es Salaam. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Leonard Akwilapo akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Shirika la Un Habitat for Humanity Tanzania wakati wa sherehe za miaka 40 ya shirika hilo zilizofanyika jijini Dar es Salaam.  Wa pili kushoto ni Mlezi wa shirika hilo mama Anna Mkpa (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)

Wed, 30 Sep 2026 15:51:34 +0000
Uncategorized · Business Daily

The Kenyans making money from chasing waterfalls

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Ebola en RDC : l’OMS appelle à renforcer l’accès à l’oxygène et aux soins

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · The Observer Uganda

Why Makerere’s $10,000-scientist drive aims to shield Africa from pandemics

When COVID-19 swept across Africa, public health officials faced a humiliating reality. As local health centres filled, African epidemiologists and governments were forced to rely…

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Top 25 countries by English proficiency

Singapore ranks second overall with a score of 631.

Recently
Uncategorized · Issa Michuzi

TANZANIA, ALGERIA ZAPIGA HATUA ZA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA TANO

ALGIERS: Tanzania na Algeria zimepiga hatua katika kuimarisha ushirikiano katika sekta tano muhimu, huku nchi hizo zikitarajia kupanua ushirikiano huo katika maeneo mengine kwa lengo la kuleta manufaa kwa wananchi wa pande zote mbili. Hayo yamesemwa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Mobhare Matinyi, wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya Algeria leo asubuhi katika ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers. Balozi Matinyi amesema sekta ambazo zimepiga hatua katika kipindi cha miezi michache iliyopita ni viwanda vya dawa, nishati, elimu ya juu, biashara ya mazao ya kilimo na ufugaji wa nyuki. Amesema hatua hizo zinafuatia maelekezo ya viongozi wa nchi hizo mbili ya kugeuza maeneo ya ushirikiano yaliyobainishwa kuwa fursa halisi za maendeleo kwa wananchi. “Nilipowasilisha hati zangu za utambulisho mnamo Juni 10, 2026, Rais Abdelmadjid Tebboune alisisitiza kwamba sasa umefika wakati wa kuuweka ushirikiano wetu katika vitendo. Nilipokuja Algeria, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pia alisisitiza kwamba kutokana na ushirikiano wetu wa kimkakati, sasa ni wakati wa kupata manufaa kwa ajili ya wananchi wetu,” amesema Balozi Matinyi. Ushirikiano katika dawa Akizungumzia sekta ya dawa, Balozi Matinyi amesema Mamlaka ya Taifa ya Bidhaa za Dawa ya Algeria (ANPP) pamoja na Saidal Group, kampuni ya dawa inayomilikiwa na Serikali ya Algeria, zinatarajiwa kufanya ziara nchini Tanzania mwezi Oktoba kwa mwaliko wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA). Amesema ziara hiyo inalenga kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu kati ya taasisi hizo. Ameeleza kuwa Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kufikia kiwango cha juu cha ML3 katika mfumo wa ukaguzi wa dawa mwaka 2018, kwa mujibu wa tathmini ya Shirika la Afya Duniani (WHO), huku Algeria ikiwa na takribani theluthi moja ya viwanda vya dawa vilivyopo barani Afrika. Balozi Matinyi amesema hali hiyo inaweka msingi mzuri wa nchi hizo mbili kushirikiana na kufikia mafanikio makubwa katika sekta ya dawa. Aidha, amesema kampuni ya dawa ya Hikma iko katika hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano ya ushirikiano katika biashara na uwekezaji na Medipharm, kampuni tanzu ya Bohari Kuu ya Dawa (MSD), kwa lengo la kuhudumia masoko ya nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini. Amesema kampuni nyingine ya Algeria, Frater Razes, inatarajiwa kufika Tanzania mwezi Oktoba kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Serikali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji. Nishati Katika sekta ya nishati, Balozi Matinyi amesema Kampuni ya Usafirishaji na Usambazaji Umeme (ETDCO), kampuni tanzu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), ilifanya ziara nchini Algeria mwezi Julai kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano wa kiufundi. Amesema wakati wa ziara hiyo, wataalamu wa ETDCO walitembelea maeneo ya kiufundi ya Shirika la Umeme na Gesi la Algeria (SONELGAZ), pamoja na kiwanda cha vifaa vya umeme cha GISB Electric. Algeria kutoa nafasi 176 za masomo Katika sekta ya elimu ya juu, Balozi Matinyi amesema Algeria imetoa nafasi 176 za masomo ya juu kwa wanafunzi kutoka Tanzania. Amesema Serikali ya Tanzania imeamua kuchagua wanafunzi 150 wenye ufaulu wa juu chini ya mpango wa Samia Scholarship Extended, ambao wataenda kusoma masomo ya sayansi, teknolojia, uhandisi na tiba nchini Algeria. Korosho na usindikaji wa mazao Akizungumzia biashara ya mazao ya kilimo, Balozi Matinyi amesema kampuni ya Algeria ya Sarl Anacard’Or imenunua ghala la kuhifadhia korosho mkoani Mtwara kwa ajili ya kurahisisha usafirishaji wa korosho kwenda Algeria. Amesema kampuni hiyo pia iko katika hatua za kukamilisha mipango ya kuanza shughuli za ubanguaji wa korosho nchini Tanzania. Aidha, amesema kampuni nyingine ya Algeria inayotengeneza mashine za kusindika mazao ya kilimo, dawa na vifaa vya kufungashia, CAM Sarl, imekubali kushirikiana na Tanzania katika upatikanaji wa mashine hizo kwa ajili ya kuongeza thamani ya mazao kabla ya kupelekwa katika masoko ya kimataifa. Ushirikiano katika ufugaji wa nyuki Balozi Matinyi amesema Tanzania na Algeria pia zinatarajia kuanza ushirikiano katika sekta ya ufugaji wa nyuki na mazao yake. Amesema hatua hiyo imefuatia ziara ya maafisa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mamlaka ya Huduma za Misitu Tanzania (TFS) pamoja na wadau wa sekta binafsi nchini Algeria mwezi Septemba 2026, ambapo pande hizo zilikubaliana kuanza ushirikiano katika eneo hilo. Akihitimisha mazungumzo yake na waandishi wa habari wa Algeria, Balozi Matinyi amewakaribisha wananchi wa Algeria kutembelea Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii, ikiwemo Hifadhi za Taifa za Serengeti na eneo la Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro pamoja na fukwe za Zanzibar.

Wed, 30 Sep 2026 16:02:17 +0000
Uncategorized · PML Daily

Ugandan tour firms use virtual reality to sell safaris in Addis Ababa

Ugandan tour operators have used virtual reality to promote the country to visitors at a regional tourism fair in Ethiopia, as Uganda seeks to grow arrivals from what officials call a...

Recently
Uncategorized · The Star Kenya

Botswana faces backlash over 23 elephant killings

A licence issued by the government authorises the hunting of 23 elephants and other wild animals for "complimentary purposes".

Recently
National · Issa Michuzi

KIHONGOSI AAWASILISHA TAARIFA YA MAFUNZO YA ITIKADI NA UJENZI WA CCM

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi, amewasilisha taarifa kuhusu mafunzo ya kuongeza uelewa wa itikadi ya CCM, ujenzi wa Chama na kuongeza wanachama wapya, yaliyohitimishwa leo Septemba 30, 2026, katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Tunguu, Zanzibar. Mafunzo hayo ya awamu ya pili yamehitimishwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Akizungumza katika hafla hiyo, Kihongosi amesema usaili wa makada waliohudhuria mafunzo hayo ulizingatia uelewa wa historia, muundo, misingi na itikadi ya CCM, uwezo wa kujenga na kuwasilisha hoja, mbinu za ufundishaji, maadili na nidhamu, pamoja na uwezo wa kuendeleza elimu ya Chama. Amesema mfumo huo wa usaili umewezesha kuweka viwango vinavyofanana vya uteuzi kabla ya makada hao kuanza mafunzo. Kwa mujibu wa Kihongosi, mchakato huo wa usaili umekamilisha hatua muhimu ya udhibiti wa ubora kwa kuunganisha viwango vya uteuzi katika mikoa 32 na wilaya 168. Amesema mafunzo hayo yamejikita katika maeneo mbalimbali, yakiwemo muundo na historia ya CCM, misingi na itikadi ya Chama, maadili katika itikadi na falsafa ya CCM, ujenzi wa makada, ujenzi upya wa imani ya wanachama na wananchi, pamoja na uwezo wa kujenga hoja. Aidha, amesema mafunzo hayo yamezingatia matumizi ya mazingira ya kidijitali katika utoaji wa elimu na mawasiliano ya kisiasa, hatua inayolenga kuwawezesha makada kuendana na mabadiliko ya teknolojia na mazingira ya sasa ya mawasiliano.

Wed, 30 Sep 2026 15:52:01 +0000
Uncategorized · DW Afrique

Élèves filmés en classe : le ministère ivoirien met en garde

Read the full report from the original source.

Recently

Page 955 of 1131 · 22611 stories