Unganishwa

Search the region

22611 stories

Uncategorized · UN News Burundi

Funding cuts put 8.3 million refugees at risk of losing vital assistance

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Capital FM

Kamukunji MP Yusuf Hassan urges Govt to settle Sh23mn Morocco mission bills

Latest · Business

Recently
National · Issa Michuzi

CP MKAMA AWATAKA MAAFISA HABARI WA POLISI KUWA WABUNIFU

Kamishna wa Polisi Jamii, CP Alex Mkama, amewataka Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kutumia maarifa waliyoyapata katika mafunzo kuboresha utendaji wao na kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika tasnia ya habari. CP Mkama ametoa kauli hiyo wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Habari wa Jeshi la Polisi kilichofanyika katika Chuo cha Polisi Tanzania, Moshi, kuanzia Septemba 28 hadi 30, 2026. Amesema mafunzo hayo yanapaswa kutafsiriwa kwa vitendo katika maeneo yao ya kazi, akiwataka Maafisa Habari kuwa wabunifu, hususan katika matumizi ya mitandao ya kijamii, ili kufikisha taarifa kwa wananchi kwa haraka, usahihi na kwa wakati. Aidha, amewataka Maafisa Habari hao kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi, uadilifu na uzalendo, huku wakitambua wajibu wao katika kulinda na kuimarisha amani ya Jeshi la Polisi na nchi kwa ujumla. CP Mkama pia amewataka kuendelea kuboresha utendaji wao katika tasnia ya habari kwa kutumia maarifa na ujuzi walioupata, akisisitiza umuhimu wa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kuhakikisha hawamwangushi Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania.

Wed, 30 Sep 2026 15:43:11 +0000
Uncategorized · BBC Afrique

Ce que l'on sait de l'agression au couteau à bord d'un vol Flydubai à destination d'Israël

Le commandant de bord et le copilote ont été blessés, et un pilote a été arrêté, selon les autorités.

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

NABALEMA ANGELA: The youth vision belongs to those prepared to innovate

The world is changing at a remarkable pace. Technology, new ideas and evolving social needs are transforming the way people work, communicate, learn and solve problems. In such an environment,…

Recently
Uncategorized · Watchdog Uganda

Minister Babalanda tasks Greater Masaka RDCs, DISOs to strengthen monitoring, accountability

The Minister for the Presidency, Hon. Babirye Milly Babalanda, has tasked Resident District Commissioners (RDCs), Resident City Commissioners (RCCs) and security officials in the Greater Masaka sub-region to strengthen f

Recently
Uncategorized · PML Daily

Museveni backs Dangote’s Lamu refinery, says Uganda will still build its own

President Yoweri Museveni has welcomed plans for a 700,000-barrel-per-day oil refinery in Kenya and called for more refineries across East Africa, saying the region should process its own natural resources to...

Recently
Uncategorized · Capital FM

Sakaja, Residents’ Associations Strengthen Nairobi El Niño Flood Response

Latest · NATIONAL NEWS

Recently
Business · Issa Michuzi

Benki ya NBC Yatambulisha Msimu wa Tano Kampeni ya NBC Shambani Mtwara, DC Tandahimba Asisitiza Wakulima Kuweka Akiba

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua msimu wa tano wa kampeni yake ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde, Tunakuona Mbali Mkulima” katika mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, ikiwa na lengo la kuimarisha elimu ya fedha, matumizi ya huduma rasmi za kifedha na kuongeza tija katika kilimo, hususani zao la korosho. Uzinduzi huo ulifanyika Mtwara ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Mstaafu Michael Mtenjele, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Donald Msengi, na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima na viongozi waandamizi wa NBC, akiwemo Mkurugenzi wa Wateja Wadogo, Elibariki Masuke, Mkuu wa Masoko, David Raymond, Meneja wa Kanda ya Pwani, Zubeider Haroun, na Mkuu wa Kitengo cha Wakulima, Raymond Urassa. Akizungumza katika hafla hiyo, Kanali Mstaafu Mtenjele aliipongeza NBC kwa kuwawezesha wakulima kupitia huduma za kifedha na elimu ya fedha, akisema utamaduni wa kuweka akiba ni muhimu kwa maendeleo ya mkulima, familia na uchumi wa taifa. “Wakulima wanapaswa kuwa na utamaduni wa kuweka akiba. Akiba si kwa manufaa ya mkulima na familia yake pekee, bali pia ina mchango katika ukuaji wa uchumi wa taifa,” alisema Mtenjele. Alisema huduma kama bima ya afya zina umuhimu mkubwa kwa wakulima kwa kuwa kipato chao kinategemea misimu ya uzalishaji, huku elimu ya fedha ikiwa muhimu katika kuwawezesha kupanga matumizi, kununua pembejeo na kuwekeza katika shughuli zao. Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke, alisema kampeni hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki kuitikia ajenda ya Serikali ya 10/30, inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kutoka asilimia 5 hadi asilimia 10 ifikapo mwaka 2030. “Kilimo ni biashara, na kwa kutambua hilo tunaendelea kubuni bidhaa na huduma zinazokidhi mahitaji ya mkulima ili kumwezesha kuongeza uzalishaji, kusimamia mapato yake na kuwekeza zaidi katika shughuli za kilimo,” alisema Masuke. Alisema NBC imeendelea kubuni huduma zinazokidhi mahitaji ya wakulima, ikiwemo akaunti za NBC Shambani zisizo na makato ya kila mwezi, bima ya mazao na afya, huduma za uwakala na kidigitali, mikopo ya pembejeo, mikopo ya matrekta na malori kwa AMCOS, ujenzi wa maghala pamoja na malipo ya awali kupitia stakabadhi ghalani. Masuke alisema kampeni hiyo imeleta mabadiliko katika matumizi ya huduma rasmi za kifedha mkoani Mtwara, akibainisha kuwa wakulima wengi sasa wanaweka fedha zao benki, wanatumia huduma za kidigitali na kujiunga na bima za mazao na afya. “Tunajivunia kuona fedha za wakulima sasa zikitulia benki, huku wengi wakianza kutumia huduma za kidigitali na kuchukua bima za mazao na afya. Haya ndiyo mabadiliko tuliyokusudia kuyafikia kupitia kampeni hizi,” alisema. Kivutio kikubwa cha msimu huu ni mfumo wa zawadi unaowahusisha wakulima mmoja mmoja, AMCOS na vyama vikuu vya ushirika (Unions). Wakulima mmoja mmoja watapata nafasi ya kujishindia baiskeli na pikipiki, AMCOS zikiwania mashine za kufungia mifuko, huku vyama vikuu vya ushirika vikishindania magari mawili aina ya double cabin pickup. Ili kushiriki, wakulima, AMCOS na Vyama Vikuu vya Ushirika wanatakiwa kufungua akaunti ya NBC Shambani na kupitisha fedha zao kupitia akaunti hizo, huku zawadi zikitolewa kila mwezi. Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Masasi-Mtwara (MAMCU), Biadia Matipa, aliipongeza NBC kwa kurejesha thamani kwa wakulima kupitia kampeni hiyo, akisema MAMCU imejipanga kushiriki kikamilifu na kuwania zawadi kuu ya gari la double cabin. “Tumejipanga kuhakikisha tunanufaika na zawadi hizi, na nina uhakika zawadi hii kuu ya gari la double cabin itakuja MAMCU,” alisema Matipa. Naye Mwenyekiti wa RUNALI na KCJE Ltd, Odas Mpunga, alisema kampeni hiyo imeongeza uelewa wa wakulima kuhusu huduma za kifedha kupitia mawakala wanaowafikia moja kwa moja vijijini. “Bima ya afya ni muhimu kwa mkulima kwa sababu afya ndiyo inayomwezesha kufanya kazi kwa ufanisi. Pia mashine za kushonea mifuko zitatusaidia sana AMCOS katika shughuli za kuhifadhi korosho,” alisema Mpunga. Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Wakulima wa NBC, Raymond Urassa, alisema kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa kuhusu bima, mikopo, huduma za mawakala na huduma za kidigitali, akiwataka wakulima kutumia huduma hizo badala ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika matawi ya benki. “Tunataka mkulima aweze kupata huduma za benki akiwa karibu na shughuli zake za uzalishaji. Matumizi ya mawakala na huduma za kidigitali yanamsaidia kuokoa muda na gharama za kusafiri kwenda kwenye matawi,” alisema Urassa. Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza, alisema kampeni hiyo itasaidia kuongeza ushiriki wa wakulima katika mfumo rasmi wa kifedha na kuimarisha ushirika. “Kampeni hii ni fursa nzuri ya kuwashawishi wakulima zaidi kuingia kwenye huduma rasmi za kibenki na kuimarisha ushiriki wao katika vyama vya ushirika,” alisema Nsunza. Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Mstaafu Michael Mtenjele (katikati), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa msimu wa tano wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde, Tunakuona Mbali Mkulima” katika mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Kampeni hiyo inalenga kuimarisha elimu ya fedha, matumizi ya huduma rasmi za kifedha na kuongeza tija katika kilimo, hususan zao la korosho, huku ikiwapa wakulima fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo magari mawili aina ya double cabin pickup kwa vyama vikuu vya ushirika katika mikoa hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika Mtwara jana na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima na viongozi waandamizi wa NBC. Wengine ni viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima na viongozi waandamizi wa NBC. Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Mstaafu Michael Mtenjele (katikati), akimpongeza Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke (kulia), wakati wa hafla ya uzinduzi wa msimu wa tano wa kampeni ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde, Tunakuona Mbali Mkulima” katika mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Kampeni hiyo inalenga kuimarisha elimu ya fedha, matumizi ya huduma rasmi za kifedha na kuongeza tija katika kilimo, hususan zao la korosho, huku ikiwapa wakulima fursa ya kushinda zawadi mbalimbali, zikiwemo magari mawili aina ya double cabin pickup kwa vyama vikuu vya ushirika katika mikoa hiyo. Uzinduzi huo ulifanyika Mtwara jana na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima na viongozi waandamizi wa NBC. Kushoto ni Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza. Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Kanali Mstaafu Michael Mtenjele (ndani ya gari), akipima ubora wa gari aina ya double cabin pickup itakayotolewa na benki ya Taifa ya biashara (NBC) kama zawadi kwa washindi wa kampeni yake ya “Wekeza NBC Shambani Ushinde, Tunakuona Mbali Mkulima” katika mikoa ya Mtwara na Lindi pamoja na Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma. Kampeni hiyo inalenga kuimarisha elimu ya fedha, matumizi ya huduma rasmi za kifedha na kuongeza tija katika kilimo, hususan zao la korosho. Uzinduzi wa kampeni hiyo ulifanyika Mtwara jana na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama vya ushirika, wakulima na viongozi waandamizi wa NBC. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Robert Nsunza (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha Wakulima wa NBC, Raymond Urassa (kushoto) Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Wakulima wa NBC, Raymond Urassa (pichani) alisema kampeni hiyo inalenga kuongeza uelewa kuhusu bima, mikopo, huduma za mawakala na huduma za kidigitali, akiwataka wakulima kutumia huduma hizo badala ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma katika matawi ya benki. Katika hafla hiyo maofisa wa benki ya NBC walipata wasaa wa kuwajengea uelewa zaidi wakulima wa korosho kuhusu elimu ya fedha na huduma mbalimbali za benki hiyo ikiwemo huduma ya bima za afya na bima za kilimo. Wakulima walishiriki kikamlifu hafla hiyo. Kivutio kikubwa cha msimu huu ni mfumo wa zawadi unaowahusisha wakulima mmoja mmoja, AMCOS na vyama vikuu vya ushirika (Unions). Wakulima mmoja mmoja watapata nafasi ya kujishindia baiskeli na pikipiki, AMCOS zikiwania mashine za kufungia mifuko, huku vyama vikuu vya ushirika vikishindania magari mawili aina ya double cabin pickup.

Wed, 30 Sep 2026 15:34:28 +0000
National · Issa Michuzi

GST YATOA ELIMU YA MAJANGA, JIOLOJIA NA EL NINO MAMBA MIAMBA SAME

Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imetoa elimu kuhusu tahadhari za majanga ya asili, masuala ya jiolojia na El Nino kwa wakazi wa Kijiji cha Mamba Miamba, Jimbo la Same Mashariki, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. Elimu hiyo imetolewa leo katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa Serikali ya Kijiji, Mtendaji wa Kijiji pamoja na wananchi, ambapo wamejadili hatua mbalimbali za kuchukua ili kupunguza athari za majanga ya asili katika eneo hilo. Kikao hicho kimefanyika kufuatia ombi la Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, alilolitoa Septemba 28, 2026, baada ya semina iliyowakutanisha maafisa tarafa, madiwani na watendaji wa kata. Katika semina hiyo, pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo hatarishi yaliyopo upande wa tambarare, mbunge huyo aliwaomba wataalamu kufika maeneo ya milimani kwa ajili ya kutoa elimu na ushauri wa kitaalamu kwa wananchi. Katika kikao hicho, wananchi wamekubaliana kusitisha mara moja shughuli za kilimo katika eneo lililowahi kuathiriwa na maporomoko ya udongo mwaka 2009. Badala yake, wamekubaliana kupanda miti katika eneo hilo ili kusaidia kurejesha uimara wa udongo na kupunguza mmomonyoko. Aidha, wananchi wameiomba Serikali kuchukua hatua za kudhibiti athari za radi katika eneo hilo, ikiwemo kuweka mifumo au vifaa maalumu vya kinga dhidi ya radi, kutokana na eneo hilo kuwa na historia ya kukumbwa na matukio ya radi mara kwa mara. Wataalamu wa GST wamewasisitiza wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa na mamlaka husika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na majanga ya asili, pamoja na kuchukua hatua mapema wanapoona dalili zinazoweza kuhatarisha usalama wa watu na mali. GST imeendelea kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali nchini kuhusu masuala ya jiolojia, majanga ya asili na namna ya kuchukua tahadhari, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuongeza uelewa wa wananchi na kupunguza athari za majanga yanayoweza kujitokeza.

Wed, 30 Sep 2026 15:39:28 +0000
Uncategorized · KT Press

Rwanda Government May Be Forced to Increase Diesel Subsidy to Keep Price Down

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Business Daily Africa

Asahi sees EABL growing with premium beer brands

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · BBC Afrique

Dans une ville de première ligne au Yémen, les Houthis luttent pour le contrôle

Exceptionnellement, la BBC a accédé à la zone de conflit au Yémen et s'est rendue sur la ligne de front avec des soldats progouvernementaux.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

La MONUSCO a rapatrié 122 ex-FDLR vers le Rwanda en Septembre 2026

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KT Press

Rwanda’s Improving Audit Record Faces New Generational Risks

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KT Press

As HealthTech Expands, Africa Faces the Challenge of Scaling Innovation

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KT Press

Five Years On, Rwanda Is Leading the Edge of Digital Health in Africa

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Citizen Digital

Kakamega OCS charged with allegedly defiling 14-year-old girl

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · KBC

Tax polluters to finance Africa’s climate action, Wetang’ula urges

Read the full report from the original source.

Recently
Uncategorized · Rwanda News Agency

Le président de la FERWAFA Fabrice Shema Ngoga démissionne

Read the full report from the original source.

Recently

Page 956 of 1131 · 22611 stories